Tick Tock. Tick Tock. Kwa nini saa yangu halisi imeharikiba hivyo?

Soma kipande hiki hapa chini ili uelewe mgeni wako wa kila mwezi vizuri zaidi!

Jina langu ni Zama na nipo hapa kuwazungumzia kuhusu suala nyeti sana kwa msichana: HEDHI! Kitu hicho kinamtendekea kila msichana katika dunia nzima, lakini tunapaswa kuaibika zaidi kukizungumzia.

Dada, huo ni upuzi.

Kwa hivyo wacha tuzungumzie vitu vichache ambavyo vimetufanya kuwa waoga sana kuzungumzia. Ni mili yetu, na ni wajibu wetu kujua jinsi inavyofanya kazi. Kitu tu kinachoogofya kuhusu kuwa na hedhi ni kutojua kinachotendeka unapoipata:

Myriella kutoka Kongo: “Tayari nimefikisha miaka 15! Na bado sijapata hedhi yangu. Marafiki zangu wote wananicheka, wakiniambia bado mimi ni mtoto. Niko sawa?”

Kwanza, ndiyo. Uko sawa. Uko salama! Tulia.

Wasichana kwa kawaida huanza kupata hedhi takribani miaka 2 baada ya kuvunja ungo. Ishara za kuvunja ungo ni kuota matiti lakini wakati mwingine nywele za sehemu za siri huota kwanza. Ni jambo la kawaida kuota nywele za kwapani au ‘za huko chini’ kabla hujaanza kupata hedhi zako!

Unaweza pia kumwuliza mama yako umri aliokuwa nao alipopata hedhi yake ya kwanza, kwa sababu mambo kama hayo yanaweza kuwa ya kurithi. Sababu nyingine: wasichana ambao ni wanariadha sugu au ni wembamba sana huchelewa kupata hedhi, na baadhi ya wasichana hawapati hedhi zao kwa sababu ya tofauti ya homoni. Msongo mkubwa wa mawazo? Hilo pia.

Abia kutoka Moroko: “Lakini nina wasiwasi. Itakuwaje nisipopata hedhi zangu?”

Wasichana wanaofikisha umri wa miaka 16 bila kupata hedhi huenda wakawa na ukosefu wa mtiririko wa hedhi. Ninapendekeza umwambie mama yako kuhusu tatizo hili na kuomba ushauri wa daktari ili kufanyiwa vipimo vya matibabu na utambuzi wa ugonjwa!

Sara kutoka Visiwa vya British Virgin: “Nina miaka 22 na ninatambua kuwa kuna mzunguko usio wa kawaida wa hedhi zangu. Hata ninapata hedhi mara mbili kwa mwezi na huwa nzito sana! Nisaidie!”

Kwa wastani, mwanamke atapata hedhi zake siku 3 hadi 7 mara moja kwa mwezi. Lakini kiasi cha damu inayotoka wakati wa hedhi kinatofautiana. Baadhi ya wanawake hupata hedhi nzito sana kuliko wengine. Hizi hapa ni baadhi ya sababu za hedhi zisizo za kawaida:

  • Msongo wa mawazo. Ni sababu kuu ya hedhi zisizo za kawaida! Fahamu homoni inayokupa msongo wa mawazo: Kotisoli. Ikiwa una kotisoli kupita kiasi katika mkondo wako wa damu, wakati na mtiririko wa mzunguko wako unaweza kubadilika! Wasichana, mjipende na kujitunza.

  • Lishe. Lishe huathiri karibu kila kitu kuhusu jinsi mwili wako unavyofanya kazi, na hiyo inajumuisha mzunguko wako wa hedhi. Ikiwa ulihitji sababu nyingine ya kuepuka mafuta mengi, sukari nyingi, kula mboga kwa uhuru... sasa unayo!

  • Mazoezi. Ili kupata hedhi ya kawaida, mwili wako unahitaji kuwa na kiwango fulani cha mafuta na madini. Ikiwa unafanya mazoezi kwa bidii (kwa bidii haswa!) kwa ajili ya spoti, wakati mwingine hii inaweza kusimamisha hedhi yako kuja kawaida.

Na mwisho ila si mwisho kabisa: usiwahi kuogopa kutafuta majibu. Ukiwa na wasiwasi, mwulize mama yako. Ikiwa hajui tatizo, mwulize daktari wako. Ikiwa hajui, mwulize daktari mwingine. Ni mwili wako, ni maisha yako, na ni uamuzi wako wa kufanya.

Share your feedback