Hadithi za kweli: Jinsi hobby yangu ilivyookoa maisha yangu

Ubunifu unaweza kuongeza kujiamini

Maisha hayajakuwa rahisi kwangu tangu wazazi wangu kuaga. Nilikuwa mwana wa kipekee, na walikuwa kila kitu kwangu. Kuwapoteza wazazi wangu, nilijihisi mpweke, bila mwongozo au usaidizi - hasa katika kufanya maamuzi, kupokea ushauri na zaidi ya yote, maswala ya pesa.

Nilichukuliwa na shangazi na mjomba wangu, walionitunza kama mmoja wao. Nilithamini sana msaada na mapenzi yao. Walikuwa wema sana kwangu, lakini nilipambana kwa vile ilinibidi kuwategemea kwa kila kitu na nilihisi wasiwasi kwa hilo, wakati mwingine ninahisi nina hatia hata, hasa walipokuwa na familia yao ya kutunza.

Mchana mmoja nilikuwa na rafiki mmoja aliyekuja kunitembelea na tulikuwa tunasukana nywele jikoni. Ninapenda kusuka nyele zangu na za marafiki zangu wote - kujaribu mitindo mipya na urembo ni hobby yangu ninayopenda sana. Shangazi yangu aliona shauku na talanta yangu na akapendekeza labda ningebadilisha hobby yangu iwe mbinu ya kujipatia pesa kiasi. Alielewa nivyohisi kuhusu mambo na alitaka kunisaidia.

Sikuwa nimefikiria hivo hata kidogo - kuchukua ninachopenda kufanya na kuibadilisha iwe mbinu ya kupata pesa. Nilichangamka kutaka kuijaribu! Shangazi yangu alinisaidia kutengeneza mbinu za kutangaza biashara yangu ya kando na akanipa nafasi ya kufanya ususi nymbani kwao.

Ghafla wikendi zangu zilikuwa zimejaa maazimio - kukuza biashara yangu mpya, kuwahudumia wateja wangu wachache wa kwanza, kuhakikisha nafanya kazi nzuri iwezekanavyo. Maneno yalisambaa na nikapata uhifadhi zaidi na zaidi. Bila kujua, nilikuwa msusi maarufu mjini.

Tangu biashara yangu kuanza nimejiamini zaidi kuhusu maisha yangu na siku za usoni. Kuwa na pesa zangu mwenyewe kufanyia ninayotaka na ninayohitaji ni murua na imenipa uhuru niliohitaji.

Share your feedback