Springster hukusanya taarifa (“data”) kukuhusu ili kukusaidia kufaidi zaidi kutokana na Springster na bidhaa zingine zinazohusishwa nasi. Tunapokusanya data yako, sisi huhakikisha kwamba imewekwa salama na tunaheshimu usiri wako nyakati zote (unapotumia tovuti ya Springster na vilevile kama utaacha kuitumia).
Tumejitolea kukupa usalama huu na usiri nyakati zote, pia tunahitajika kufanya hivyo chini ya sheria mbalimbali (kama vile sheria kuhusu Ulinzi wa Data na usiri) zinazotumika katika Girl Effect (‘mama’ wa Springster), kwa kuwa ofisi yetu kuu iko Uingereza.
Taarifa ambazo tunakusanya kutoka kwako.
Ukijisajili kutumia Springster, bila kujali mahali ulipo kijiografia, tutakusanya na kuhifadhi taarifa fulani kukuhusu. Taarifa hizi ni pamoja na jina lako la mtumiaji (utakalolichagua mwenyewe), umri wako, jinsia yako, nenosiri lako na maswali yako ya usalama. Iwapo utashiriki katika utoaji maoni, kura na utafiti, au mashindano, tutahifadhi taarifa hizo pia. Kama unatumia programu yetu ya chatbot, vilevile tutahifadhi jina lako la Facebook katika data tutakayokusanya.
Taarifa tunazokusanya kwa kuwa unatumia Springster.
Tunaweza kukusanya taarifa kuhusu nchi yako wakati unapotumia Springster na bidhaa husika, kama vile chatbot. Zaidi ya hayo, kupitia njia zaidi za kiufundi, kama vile Vidakuzi, tunaweza pia kukusanya taarifa zaidi kuhusu mahali ulipo (kwa mfano kijiji au mji wako). (Kidakuzi ni faili ndogo ya matini ambayo hupakuliwa na kuingizwa kwenye kompyuta au simu mahiri yako unapotembelea tovuti fulani. Kidakuzi hiki huruhusu tovuti kutambua kifaa chako na kuhifadhi taarifa fulani kuhusu mapendeleo yako au vitendo vyako vya awali).
Tunatumia Vidakuzi kufuatilia vitu kama vile idadi ya watu kutoka eneo lako la jumla ambao wametumia tovuti. Hatuwezi kamwe kutumia taarifa kuhusu mahali ulipo ili kukutafuta au kutafuta nyumbani kwako isipokuwa kama umeombwa kutoa taarifa kama hii na ukatupa idhini yako kamili.
Utakapokuwa ukishiriki katika upigaji kura na utafiti, au utakapokuwa ukitumia chatbot ya Springster, tunaweza kukuomba utoe taarifa kukuhusu na maisha yako au utwambie kuhusu maoni na uzoefu wako. Unaweza kuchagua ni taarifa zipi ungependa kutoa. Tutatumia taarifa hizi kutusaidia kuhakikisha kwamba tunawapa watumiaji wa Springster huduma bora zaidi na vilevile aina muhimu zaidi za taarifa.
Data ambayo unaweza kutupatia bila sisi kuiomba.
Wakati mwingine, unaweza kujihusisha katika mazungumzo kwenye Springster au bidhaa zingine zetu. Unapotoa maoni kwenye tovuti, una chaguo la kutoa maoni yako bila kujitambulisha. Unapotoa maoni, unaweza kutoa taarifa kukuhusu, kuhusu uraibu wako, familia, mambo yaliyokutendekea, mambo ambayo ungependa kuyafanya, fikra na hisia zako. Tutafanya kila tuwezalo kufuatilia maoni haya na kuhakikisha kwamba chochote ambacho hakifai au kinachoweza kukutambulisha kimeondolewa. Lakini tafadhali kumbuka kwamba ni jukumu lako kutotoa taarifa za kibinafsi ambazo zinaweza kukutambulisha unapotoa maoni kwenye Springster. Tunatumia taarifa zilizotolewa kwenye maoni ili kuelewa vyema kuhusu mada na hadithi ambazo hupendeza watu wanaotumia Sprinster, namna watumiaji wa Springster hutumia taarifa zinazotolewa kupitia bidhaa zetu katika maisha yao ya kila siku na kuboresha huduma kama vile chatbot yetu.
Kama unatumia chatbot kupitia Facebook Messenger, taarifa utakazotoa kwenye chatbot zitahusishwa na wasifu wako wa Facebook. Taarifa hizi hazitatolewa hadharani na tutazitumia tu kusaidia chatbot kujifahamisha na kuboresha namna inavyokupa taarifa.
Watu ambao tunashiriki nao taarifa zako.
Kikundi cha kwanza cha watu ambao wanaweza kuona taarifa yoyote tuliyokusanya kutoka kwako ni wafanyikazi wa Girl Effect (na wale wanaofanya kazi kwa niaba ya Girl Effect), wote hawa wakiwa wametia sahihi makubaliano kuthibitisha kwamba watadumisha usiri wa taarifa zako na ambao wanahitajika kufuata sheria kali zinazohusiana na usiri na usalama Wafanyikazi wetu huchaguliwa kwa makini, hupewa mafunzo na wamejitolea kuwahudumia kama wanachama wa jumuiya ya Springster.
Zaidi ya hayo, wakati mwingine sisi hufanya kazi na makampuni au mashirika mengine ili kutusaidia kukuza na kudhibiti Springster. “Wahusika hawa wengine” wanaweza kufikia data yako ingawa kazi yao si kuikagua na wanakubaliwa tu kuona data yako ili waweze kutusaidia kufikia watu katika nchi ambazo tunapatikana kwa njia bora iwezekanavyo. Watu katika kikundi hiki cha “wahusika wengine” watakuwa pia wametia sahihi makubalino nasi kuhusu usiri na usalama, makubaliano yanayohusu yale wanayoweza au kutoweza kufanya na taarifa zako. Lakini tena, tunakuwa waangalifu sana kuhusu uchaguzi wa wahusika wetu wengine.
Wahusika wengine ambao sisi hushiriki data nao ni pamoja na:
Unaweza kuitisha orodha kamili ya wahusika wengine ambao tunashiriki data nao kama ungependa kujua zaidi kwa kuwasiliana nasi kupitia dataprotection@girleffect.org.
Kama unafikia Springster au chatbot yetu kupitia Facebook, au kama unaangalia Springster katika tovuti za mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Instagram, BBM au Line, unapaswa kukagua sera zao za usiri ili kuona namna wanavyotumia taarifa zako.
Unachoweza kufanya.
Unaweza kutuomba kufuta milele data yote tuliyo nayo kukuhusu, hii inaweza kumaanisha kwamba huenda usiweze tena kutumia huduma zote. Hii pia huitwa Haki yako ya Kusahauliwa. Kama hatuna sababu nzuri kabisa kuweka taarifa yoyote yako, tuna furaha kuifuta yote. Hata hivyo kuna nyakati ambazo tutatumia taairifa zako kwa madhumuni ya kupata takwimu au kufanya utafiti au kusaidia Girl Effect kufikia malengo yake ya kuwawezesha wasichana. Katika hali kama hizi, hatutafuta data yako yote. Tutaondoa tu vipengee vyote ambavyo vinaweza kukutambulisha (ambavyo pia huitwa ‘taarifa zinazoweza kumtambulisha mtu’) na kubakisha taarifa nyinginezo kwa matumizi yetu kama data isiyotambulisha mwenyewe (kumaanisha kwamba haiwezekani kukutambua). Tutakujulisha ikiwa tutafanya hivi. Unaweza kututumia barua pepe kupitia dataprotection@girleffect.org ili kuomba data yako ifutwe au kama una maswali mengine yoyote kuhusu data yako.
Unaweza pia kuomba kupokea nakala ya data tuliyo nayo kukuhusu, ikiwa tuna yoyote, au kutuomba turekebishe taarifa yoyote. Hizi pia huitwa Haki yako ya Kupata na Haki yako ya Kurekebisha. Tutajaribu kadri ya uwezo wetu kujibu maombi katika muda wa mwezi mmoja baada ya kuthibitisha utambulisho wako. Tafadhali tuandikie barua pepe kupitia dataprotection@girleffect.org na tutakutumia fomu ya kujaza ili tujue ni nini hasa ungependa tukufanyie.
Malalamishi.
Kama hujafurahishwa na namna tunavyodhibiti data yako, unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote kupitia dataprotection@girleffect.org na tutafanya kila juhudi kukujibu haraka iwezekanavyo, (na kila wakati ndani ya mwezi mmoja).