Jifunze kuweka malengo na jinsi ya kujiongezea ujuzi wa kukusaidia katika maisha ili 'wewe' uweze kuwa bora zaidi kadri uwezavyo.
Shule hutufundisha mambo mengi muhimu: hisabati, sayansi, sarufi nzuri na jinsi ya kujipatia marafiki, lakini kuna masomo mengi ya maisha unayoweza kujifunza tu katika ulimwengu halisi. Je, hizi siri za ajabu za maisha ni gani? Hebu natuongee, dada.
Kuweka malengo
Malengo ni mipango inayosaidia kutimiza ndoto zako. Haya yanaweza kuwa yale mambo unayotaka kuyatimiza unapomaliza shule, au hata unapokuwa bado ungali shuleni. Jinsi ya kuanza:
Panga bajeti
Moja ya sheria za kimsingi za maisha ni: usitumie pesa zinazozidi unazopata. Kama unaweza, anza kuweka akiba, hata ikiwa ni kwa kuanza na kiwango kidogo kabisa. Unapoamua kujinunulia kitu kwa raha zako, fikiria kwa nini unakihitaji. Usikope pesa ili kulipia kitu fulani, isipokuwa uwe unakihitaji sana au ni kitu ambacho kitakusaidia siku zako za usoni, kama kuanzisha biashara au kusoma zaidi. Wakati mwingine, jinsi unavyotumia pesa zako kunaweza kuwa ndiyo kizuizi kikubwa kinachokuzia kutimiza ndoto zako.
Tumia wakati wako kwa busara
Huenda ikaonekana kana kwamba una wakati mwingi sana, lakini hiyo si kweli kamwe. Wakati ndicho kitu muhimu zaidi utakachoweza kuwa nacho, kwa hiyo utumie vizuri. Weka malengo yako, jizatiti na ujaribu kutochangamana na watu au vitu vinavyoweza kukupotezea muda na kukudhoofisha. Kama rafiki anayependa kusengenya!
Changamana na watu wenye mtazamo chanya wanaoweza kukuhamasisha kuwa mtu mzuri zaidi, na utumie muda wako kufanya yale mambo yatakayokufanya uwe mtu mzuri zaidi !
Share your feedback