DIY: Tengeneza ramani ya ndoto zako

Furahia na uwe mbunifu na malengo yako

Kila mtu ana mipango ya wakati ujao. Mbinu bora ya kufanya mipango yako itimie ni kuwa na ramani ya ndoto zako. Hii inakusaidia uone matokeo ya ndoto zako na kuzifanya zikae za ukweli na zinazoweza kutimia.

Kabla ya kuanza, ni muhimu kuwa na malengo dhabiti. Ramani ya ndoto zako lazima iwe na picha za unachotaka kuwa, unachotaka kutimiza, maisha unayotaka kuishi na unavyotaka kuhisi siku za baadaye. umeelewa? Sawa Tuanze

Unahitaji kufanya nini:

  1. Pata karatasi ngumu au cardboard.

  2. Makasi na glue.

  3. Pata majarida au magazeti mazee.

  4. Angalia majarida yale na uchague picha zinazofanana na taswira yako bora ya siku za baadaye. Hizi zinaweza kuwa picha za watu wanaokuhamasisha, maeneo ungependa kutembelea, mambo unayofurahia kufanya, kazi yako unayotamani. Ramani ya ndoto zako ni ya kibinafsi kwa hivyo hakuna picha iliyosawa na isiyosawa. Waza mambo makubwa ya kuthubutu iwezekanavyo.

  5. Kata picha zinazokuhamasisha na uzibandike kwenye karatasi ngumu iliyonayo.

  6. Tafuta au andika nukuu za kutia motisha na uzibandike kwenye ramani ya ndoto zako.

  7. Bandika ramani ya ndoto zako inapoonekana, utakapoiona kila siku na ikukumbushe malengo yako kama vile kwenye ukuta wa chumba chako cha kulala au mlangoni.

Si hii ni rahisi na inaleta raha? Wakati wako kuijaribu.

Sote tuna ndoto za siku za baadaye tunazotaka lakini hazitimii pekee yake. Tunahitaji kufanya bidii na kung'ang'ana. Ramani ya ndoto itakusaidia uwe na mtazamo mzuri wa siku zako za baadaye na ikukumbushe usife moyo wakati mambo ni magumu.

Share your feedback