Vaa uvutie

Vaa kwa ajili ya kazi unayotaka, si kazi uliyo nayo!

Una mahojiano ya kazi yako ya kwanza wiki ijayo na hujui nguo unayofaa kuvaa? Usiwe na wasiwasi tena kwa sababu tutakushughulikia! Huu hapa ni mwongozo wa kuchanganya na kulinganisha vazi lako la kazini!

Shati jeupe la kawaida
Kabla hujatumia pesa za jitihada zako kununua vazi la kazi, angalia kabati lako. Una shati moja jeupe la vifungo, sivyo? Ikiwa unalo, mambo sawa! Shati jeupe ni salama zaidi na muhimu kuvaa kuenda kazini. Unaweza kuvaa nguo za kawaida na za kitaalamu kwa shati moja jeupe tu.

Kitu kilichoazimwa
Unajikimu kibajeti lakini bado unahitaji kuenda kwenye mahojiano. Huna muda wa kuenda kununua. Utafanya nini? Ni rahisi zaidi, una mshauri wa mtindo ambaye umemjua tangu siku uliyozaliwa! Nenda kwenye kabati la mama au shangazi yako na ujitayarishe kupata hazina zinazovutia na za kisasa! Hujui haswa utakachokipata. Kuanzia blauzi za kawaida maridadi hadi makoti meusi, mama ana kila kitu! Lakini hakikisha kuwa unauliza wakati wote.

Nunua kitu kinachovutia!
Ikiwa kwa kweli unahitaji kununua, basi nunua kama mtaalamu wa baadaye. Nunua nguo ambazo hazina muda wa mwisho badala ya vitu vinavyovuma. Tumia rangi za msingi, kama bluu iliyokolea, kijivu na nyeusi. Jaribu mchanganyiko huu: shati jeupe, sketi nyeusi yenye urefu wa kati, viatu vya kahawia vya mtindo! Wewe huyo sasa, mwonekano maridadi wa papo hapo! Nunua kwa busara kwa kutembelea maduka yako ya karibu pia.

Vaa kwa ajili ya ufanisi
Na ukumbuke kanuni nambari moja: kitu muhimu zaidi unachoweza kuvaa kwa ajili ya mahojiano ya kazi ni ujasiri na uwezo wako. Fahamu malengo yako wakati wa mahojiano, fanya utafiti kwa kina kuhusu cheo unachohojiwa kwacho, na usiogope kuuliza maswali. Hata ikiwa hufahamu kwa asilimia 100 kuhusu mavazi yako, ukiwa asilmia 100 kujihusu, hayo ndiyo mavazi bora ambayo umewahi kuvaa.

Kila heri, msichana!

Share your feedback