Pata motisha kutoka kwa watu hawa wanne jasiri…
Viatu vya Afrika
Mghana Mabel Suglo alikuwa na nyanya yake aliyeugua ugonjwa wa ukoma. Mabel alitaka kumtengenezea jozi la viatu vya kumrahisishia kutembea ambavyo vingedumu, kwa hiyo alijaribu kutengeneza kwa kutumia tairi za zamani na viatu vikawa maarufu zaidi. Hali hii ilimfanya Mabel kuamua kuanzisha mpango wake, Mradi wa Eco-Shoes, kutengeneza viatu na vifuasi kwa kutumia tairi za zamani na nyenzo za kutumika tena. Mabel aligundua kuwa watu wengine wenye ulemavu katika jumuiya yake mara nyingi hawakujumuishwa katika fursa, kuupuzwa au hata kuumizwa na wengine na kwa sababu hiyo, yeye huwajaari watu wenye ulemavu ili kuwapa fursa sawa.
Balozi wa Eco
Samah al-Gadi alishinda tuzo ya msimu wa kwanza wa kipindi maarufu cha Televisheni cha Kisudani Mashrouy, kwa wajasiriamali wadogo mwaka wa 2013. Aliwapiku washindani 12 kwa wazo lake linalojali mazingira –ili kuzisaidia jamii kuishi kando kando ya mto wa Nile kwa kuondoa gugumaji, ambalo husababisha kukua kwa vimelea na kuharibu makazi ya samaki. Wanajamii wangetumia gugumaji kutengeneza mifuko, samani na kamba za kuuza. Samah alijipatia $20 000 kwa ushindi wake katika shindano hili na pia ikawapa motisha wanafunzi wa kike wa Kisudani kuzingatia zaidi masomo yao. Kwa sasa, mradi wa Samah unatekelezwa jijini Khartoum.
Kuwawezesha Wasichana
Kutana na Lebogang Maruapula kutoka Botswana. Lebogang alitaka kusababisha athari chanya kila wakati katika jumuiya yake na kuwainua wasichana. Alianzisha miongoni mwa watu wengine Wakfu wa The Goddess (vuguvugu ambalo huwashauri na kuwaelimisha wanawake wadogo) na kujisajili kama balozi wa eneo wa Girl Rising (shirika la kimataifa la kutoa hamasisho kuhusu fursa sawa kwa wasichana). Mwaka wa 2014, Lebogang alikuwa mshirika katika Ushirika wa Mandela Washington kwa Viongozi Wachanga wa Kiafrika. Yeye pia ni mfanyakazi wa kujitolea katika United Nations Online na mwanaharakati katika Pacific Youth Media ya UNICEF.
Paa Juu
Mwaka wa 2005, Mwafrika Kusini Refilwe Ledwaba alikuwa mwanamke wa kwanza wa kiafrika kujipatia leseni ya rubani wa helikopta katika nchi yake na mtu wa kwanza wa kiafrika kuendesha ndege kioparesheni kwa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini. Rubani huyu, mjasiriamali wa kielimu na kijamii alianzisha pia shirika lisilo la faida, Southern African Women in Aviation and Aerospace (SAWIA) ambalo huandaa Mpango wa kila mwaka wa Girl Fly katika Afrika – kambi ya wasichana 150 wa shule ya upili wanaovutiwa na sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati (STEM), unaongazia teknolojia ya anga na elimu ya kuendesha ndege. Refilwe alishinda tuzo ya mwaka wa 2012 ya Shirika la Afrika Kusini la Ukuaji wa Vijana na mwaka wa 2014 alijumuishwa katika Waafrika 35 Maarufu wenye umri usiozidi miaka 35 katika kutoa nafasi kwa Watu Wadogo katika Masuala ya Kimataifa.
Wanawake hawa wote wamefikiria kuhusu uwezo wao na kujiwekea malengo, hili ni jambo ambalo sisi sote tunaweza kulifanya na kupata motisha kutoka kwalo!
Share your feedback