Ukiwa umeenda au hujaenda chuoni. Unaweza kuwa na mafanikio
Ulijua kuwa watu wengi waliofaulu ulimwenguni hawakukamilisha elimu ya juu? Oprah Winfrey – mwendeshaji kipindi maarufu nchini Marekani na bilionea kwa jitihada zake aliondoka chuoni kabla ya kukamilisha ili kupata kazi aliyoitiwa; ila alirudi baadaye kupata shahada yake. Kuna watu mbalimbali wenye ufanisi kama yeye huko nje. Ikiwa hutaki kuenda chuoni au huwezi kusoma zaidi, haimaanishi kuwa huwezi kupata kazi unayoipenda! Hii hapa ni namna unavyoweza kuanza kujitahidi kupata taaluma yako unayoitamani:
1. Fahamu unachokipenda – jaribu kuangazia jambo moja au mambo mawili ambayo unafurahia kuyafanya na uanze kukuza ujuzi huo leo. Kwa mfano: ikiwa unapenda magari, unaweza kumwuliza mekanika ikiwa unaweza kumwangalia akifanya kazi au kutazama video mtandaoni kuhusu jinsi mitambo inavyofanya kazi.
2. Fanya utafiti wako – tafuta taaluma zinazohusiana na mambo unayofurahia. Unaweza kutumia intaneti kuenda kwenye maktaba au unaweza kuulizia. Ukiwa katika jiji au mji wako wa karibu, tembea ukitambua biashara/shughuli zinazohusiana na mambo unayopenda au ujuzi wako.
3. Jitangaze – Tayarisha wasifukazi wako na uanze kuutuma (au ikiwa unaweza kuuwasilisha mwenyewe) kwenye kampuni au mashirika unayovutiwa nayo kuyafanyia kazi. Unaweza kuuliza kuhusu kazi, lakini pia ukufunzi, uanagenzi au kuangalia kazi inapofanywa. Ingawa huenda hizi zisilipe mara ya kwanza zitakuruhusu kujifunza. Usisahau kujumuisha barua fupi inayoelezea ni kwa nini unataka kufanya kazi hapo.
4. Jifanyie - ni nani anayesema kuwa lazima umfanyie mtu mwingine kazi? Ikiwa una kipaji au huduma ambayo watu wako tayari kulipia kwa nini ISIKUFANYE kuwa taaluma yako! Kutoka kwa bloga hadi wafumaji vikapu, washairi na madereva wa malori ulimwengu umejaa watu waliofanya kitu walichokipenda, ujuzi au kipaji kuwa biashara yenye ufanisi - na wewe pia unaweza!
5. Usitamaushwe – Fuata ndoto yako kwa kila kitu ulicho nacho. Ikiwa shahada ndicho kitu unachotaka kwa taaluma yako uipendayo, lakini haiwezekani kwako kwa sasa, haimaanishi kuwa haiko katika siku zako za usoni. Watu wengi hupata kazi ili kufadhili masomo yao au hupata msaada kutoka kwenye familia, jamii au serikali baadaye maishani.
Share your feedback