Kumpata mshauri huwa si jambo rahisi. Soma hii ili kukusaidia kwenye safari yako.
Mshauri ni mtu anayempa mwelekeo na ushauri mtu ambaye ana tajiriba ndogo. Huyu anaweza kuwa mwanamke mzee katika taaluma unayotarajia kufanya au mtu mwenye umri unaokaribiana na wako unayeenda kwake unapotafuta ushauri. Unapomtafuta mshauri bora, kumbuka mambo haya yanayofaa na yasiyofaa.
YANAYOFAA…
… Elewa aina ya mshauri unayemhitaji
Anahitaji kuwa mtu unayeweza kumwamini na ambaye amepata aina ya mafanikio unayotaka – katika maisha yake au kazi yake. Kwa kufanya hivi, ushauri na mwongozo wake unatokana na tajiriba.
… Anza na watu walio karibu nawe
Mara nyingi tayari una uhusiano na mtu ambaye unataka kujifunza kutoka kwake, labda rafiki wa familia, mkufunzi au mwanamke mfanyabiashara wa karibu. Sasa unahitaji kumwomba kuchukua jukumu rasmi zaidi maishani mwako.
… Chukua hatua
Ikiwa mshauri ni mtu ambaye humjui, basi mwandikie barua. Mwambie ni kwa nini atakuwa mshauri bora kwako. Usipopata majibu yake mara moja usikate tamaa, washauri huwa na shughuli nyingi! Fuatilia na umfahamishe kuwa bado una haja naye.
… Utafiti wako
Uliza kuhusu mipango ya ushauri kwenye kituo cha jamii, chuo au shule zilizo karibu nawe. Ikiwa huwezi kumpata mshauri, mwulize mtu mzima katika mojawapo ya maeneo haya akuongoze. Ikiwa kuna mashirika yoyote yasiyo ya serikali katika eneo lako, pia ni eneo zuri la kuanzia.
… Tumia kikamilifu kila sekunde
Muda unaotumia na mshauri wako unapaswa kuwa wenye manufaa. Jaribu kupanga mikutano wakati ambao anaweza kukupa makini yasiyotatizika na ukifanye kuwa kitu cha mara kwa mara, kama vile kila baada ya miezi michache. Kabla ya kila mkutano, andaa maswali kadhaa, mada ambayo ungependa kujadili au mapendekezo ambayo unataka majibu kuyahusu.
YASIYOFAA…
… Kuwa mbinafsi
Ili kunufaika kutoka kwa mshauri lazima ukubali mapendekezo na ukosoaji wa kukusaidia. Kuwa huru kujifunza kutoka kwake na usikubali ubinafsi wako kuingilia kati.
… Jinufaishe
Ikiwa mshauri wako ana watu wa kuwasiliana nao au anaweza kukusaidia kwa njia yoyote, kitaaluma au kibinafsi, atakufanyia hivyo. Usijaribu kujinufaishe kwa kumsukuma kutenda zaidi ya uwezo wake kwa ajili yako. Na usiwahi kumtumia kama mrejelewa bila kwanza kumwomba ruhusa.
… Tarajia mshauri wako akuokoe
Mwisho wa siku, mshauri wako hatatatua matatizo yako yote. Mchukulie kuwa rafiki, mwandani na mwelekezi.
… Kubali unyanyasaji
Mshauri mzuri hapaswi kamwe kukutamausha wala kukufanya uhisi vibaya au usiye na maana kwa njia yoyote. Hapaswi kukuomba kufanya chochote usichotaka wala kukushinikza kufanya maamuzi fulani. Unapaswa kuhisi salama, kusaidika na starehe mbele yake.
… Hisi kulazimishwa
Ikiwa huna furaha, huhisi kama unataka kuendelea kukaa na mshauri. Lakini jaribu kuwa huru kujifunza mambo mapya na uwe na kiu cha kujifunza kila mara – huo ndio wakati utakaponufaika zaidi!
Share your feedback