Mkuu wa darasa

Jifunze jinsi ya kuwa mwanafunzi bora.

Tunapaswa kufanya vyema darasani, sivyo? Bila shaka! Wakati mwingine, huwa vugumu kusoma, lakini kuna vidokezo ambavyo ni rahisi na vya kufurahia kufanya, hivyo unaweza kuongoza darasani!

Boresha Maisha Yako
Jaribu mfumo huu wa kuandika madokezo. Ukiwa shuleni, unaweza kumsikiliza mwalimu wako na kuandika taarifa muhimu katika daftari lako. Lakini unapofika nyumbani, angalia madokezo yako tena na uandike upya unachoweza ili kukusaidia kukumbuka unachoandika. Unaweza kuboresha madokezo yako ukiongeza michoro maridadi, kutumia vibandiko kurembesha madokezo yako, au kubadilisha rangi ya kalamu unayotumia. Unapopata mfumo sahihi unaokufaa, utapata motisha zaidi ya kusoma!

Wakati wa Mapumziko
Pumzisha akili zako baada ya saa moja ya kusoma, ili kujiimarisha tena. Nenda nje utembee kidogo. Hili linaweza kukutimia moyo na kukupa mwelekeo.

Jitenge na Simu Yako
Kwa kuwa unapumzisha akili zako, haimaanishi kuwa unaweza kutumia simu yako kupiga gumzo wala kucheza michezo. Si sasa hivi. Weka simu yako na vifaa vingine mbali sana nawe. Dunia haitaporomoka na hutakuwa rafiki wa ajabu kwa kuwa hujibu moja kwa moja Rafiki yako wa Dhati Daima.

Jitathmini
Mwulize ndugu, mzazi au hata rafiki yako (ambalo ni jambo zuri, kwa sababu mnashikamana na kusoma kwa wakati mmoja!) ikiwa anaweza kukutathmini. Hilo ndilo thibitisho la mwisho kwamba umesoma sana; ikiwa unaweza kukumbuka majibu ya maswali yote wanayokuuliza.

Jipe Zawadi
Bila shaka, ukipata alama ya juu kwenye tathmini yako, ni vyema kabisa kujipa zawadi. Kwa sababu ulifanya kazi nzuri! Iwe ni kuangalia Facebook yako kwa dakika chache, au kuenda kwenye jumba la biashara kwa sababu ya daraja lako la juu, fanya hivyo! Unapaswa kujivunia kile ambacho umefaulu kupata!

Share your feedback