Unataka kuanzisha biashara?

Jifundisha jinsi ya kuwashawishi watu!

Umewahi kufikiria kuhusu kuanzisha biashara? Ikiwa umewahi, utahitaji kufanya ushawishi mwingi ili kuinua biashara yako.

Kuanzisha biashara ni hatua ya kutisha na sio kila mtu atakuunga mkono, lakini usikubali hilo kukuvunja moyo! Unaweza kubadilisha mawazo ya watu na kuwafanya kukuunga mkono kwa kujifunza jinsi ya kuzungumza na kuwashawishi.

Tanya alitaka kuanzisha biashara ya kuuza bidhaa za nywele za kutengenezea nyumbani, lakini wazazi wake walitaka azingatie tu kazi yake ya shuleni. Alihitaji mkopo kutoka kwao ili kununua seti ya kwanza ya viungo, hivyo angeweza kutengeneza bidhaa na kutumia faida kununua seti zaidi.

Hii ni jinsi alivyopata kuungwa mkono na wazazi wake na kupata pesa (hivyo-tu!)

  1. Tanya aliwaza kuhusu sababu zote zinazoweza kusababisha wao kupinga, na kubuni majibu ya kabla, hivyo alikuwa tayari kwa chochote. Kwa mfano, wangedhani biashara ingeathiri matokeo shuleni. Katika jibu aliahidi kwamba ikiwa matokeo yake ya shule yangeathirika, angeweza kuacha biashara. #majadiliano

  2. Kisha, alieleza jinsi ubunifu wake ungeleta manufaa kwake na kwa familia. Wakati wote watu wanafurahishwa na mawazo ikiwa watatambua manufaa katika maisha halisi. Hivyo, Tanya aliwaeleza wazazi wake jinsi fedha za ziada zinaweza kusaidia kulipia kodi ya nyumba. Si hivyo tu, pia angeweza kujifunza mbinu zaidi ambazo zingemfanya kung’aa hata zaidi shuleni. #wazozuri

  3. Kuonyesha wazazi au walezi kuwa umeamua na uko tayari kufanya kazi kwa bidii itasaidia kuwashawishi ili kuunga mkono malengo yako. Tanya alikutana na changamoto fulani, lakini hakufa moyo. Ilichukua majaribio 20 kabla ya kufaulu kupata maagizo sahihi ya utengenezaji. #hakunakufamoyo Wazazi wake walitazama kujitolea kwake na ustahimilivu wake wakati wote katika kipindi hiki. Pia walipendezwa na kiasi cha fedha alichoweza kuhifadhi ili kuanzisha biashara.

Ilichukua muda lakini hatimaye Tanya alipata NDIYO yake! Wakati wote kumbuka kushughulikia mambo kwa utulivu na heshima wakati unataka msaada. Ikiwa utapata la, usife moyo, endelea kujaribu!

Share your feedback