Unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa?

Hapa hatua 3 kukusaidia kuanza

Unaulizwa kila wakati unataka kufanya kazi gani ukiwa mkubwa? Ahhh - linaweza kuwa swali la kufadhaisha ikiwa haujajua bado!

Usijali! Tuna hatu 3 rahisi unaweza chukua kuanza safari ya kugundua njia yako. Ndiyo, ni safari, huwezi gundua kazi unayotaka usiku kucha. Kwa hivyo kuwa mvumilivu na anza kutafuta!

1. Zingatia unachofurahia kufanya

Unapenda kuchora? Labda unaweza fikiria kuwa mchoraji. Unafurahia kusema hadithi? Waandishi wanabadilisha kusema hadithi kuwa kazi. Au labda unafurahia hesabu na kutatua matatizo? Unaweza kuwa mwanabiashara au mhasibu. Ndoto yako inafaa kuwa jambo unalofurahia kufanya - kwa hivyo fikiria hasa kuhusu unayopenda.

2. Fikiria ulilo bora kwalo

Ni vyema kuwa bora katika jambo. Inakusaidia kujenga imani yako. Kwa hivyo zingatia kama kuna ujuzi ulionao unaotaka kupeleka kiwango kingine. Uko bora katika michezo? Labda unaweza kuwa mwanariadha mtaalamu! Uko bora katika kutatua matatizo halisi? Wahandisi hutatua matatizo kupata pato lao! Wanafunzi wenza hujaa kwako kupata msaada wa kazi zao za nyumbani? Labda unaweza kuwa mwalimu!

3. Fikiria zaidi na gundua mambo mapya

Fungua macho yako na uone kazi zinazofanywa na watu karibu nawe. Unaweza kugundua sehemu mpya au kazi usiyokuwa umefikiria mbeleni. Pia kuna madara mengi ya baada ya shule na ya likizo unaweza kujaribu. Unaweza kugundua talanta usiyojua ulikuwa nayo!

Kuanza ndio jambo la muhimu. Ikiwa unajua tayari kazi unayotaka kufanya utakapokuwa... Andamana nayo! Ifuate. Ikiwa bado haujui, usishtuke. Kama tulivyosema, hii ni safari na safari huchukua muda. Unaweza chukua barabara kadhaa tofauti, lakini ukifuata moyo wako utafika ulipotaka hatimaye.

Share your feedback