Je, unajua ukweli kuhusu dawa za kulevya na pombe?

Hebu fanya zoezi la kufurahisha ili utambue unajua ukweli kuhusu dawa za kulevya na pombe kwa kiasi gani

Maelekezo

  • Utahitaji kalamu na karatasi
  • Soma kila swali, kisha andika nambari ya swali na kisha jibu kama unaona ni NGANO au UKWELI, andika kando yake
  • Bonyeza ukurasa unaofuata uone majibu
  • Jumlisha idadi ya maswali uliyojibu kwa usahihi! Ili ufurahie zoezi hili zaidi lifanye pamoja na rafiki yako kisha mlinganishe majibu yenu

Maswali

  1. Pombe si mbaya kwako kama dawa nyingine za kulevya
  2. Usingizi unausaidia mwili kuondoa pombe
  3. Mwanamke mjamzito anayekunywa pombe anahatarisha afya ya mtoto wake.
  4. Kunywa kahawa hakumsaidii mtu kutokwa na ulevi
  5. Kunywa pombe hukufanya kuwa mwerevu
  6. Dawa za kulevya hukufanya kuwa mbunifu zaidi
  7. Kufadhaika ni dalili ya mtu aliye mraibu wa dawa za kulevya
  8. Kuvuta bangi huathiri jinsi unavyotembea au kukimbia na hufanya macho yako yasiweze kuona vizuri

Je, umepata ngapi? Bonyeza hapa ujue majibu yako!

Share your feedback