Jitafutie marafiki wazuri – katika ulimwengu halisia

Je, una marafiki wengi mtandaoni kuliko wale unaowajua ana kwa ana? Jifunze kujenga mahusiano halisi leo.

Simu yako ya mkononi, intaneti, kompyuta – ni vitu vizuri sana! Unaweza kukutana watu wapya, kujifunza mambo mapya na kushiriki mawazo na marafiki kutoka duniani kote. Lakini je wale marafiki wanaoishi katika eneo lako? Intaneti ni nzuri lakini ikiwa kuwako kwako kwenye mtandao kumeleta vizuizi kati yako na marafiki zako wa kweli, huenda wakati umefika wa kuweka simu chini na kuujua ulmwengu bila #kichujio chochote!

Mazungumzo halisi

Ammera, mwanafunzi wa shule ya upili mwenye miaka 16, alituambia kuhusu siku ile alipoenda sehemu anayoipenda siku ya Jumamosi. Marafiki zake wote walikuwa huko, lakini palikuwa na kimya kingi isipokuwa milio ya simu iliyotoka kwenye simu zao. Hali ilianza kuwa ya kushangaza zaidi wakati mmoja wa marafiki zake mkubwa, aliyekuwa ameketi karibu naye alipomtumia SMS!

Huo unaweza kuonekana kuwa ni ujinga, lakini ni kitu ambacho wengi wetu wamewahi kukipitia. Ikiwa umechoka kuhisi kana kwamba uko peke yako hata unapokuwa na marafiki zako, hapa kuna wazo la kukusaidia – amua kuweka azimio kwamba mtu wa kwanza kutumia simu yake wakati mko pamoja anawaimbia watu wote wimbo wa kipuzi au anafanya kitu cha kumwaibisha. Ikiwa hilo halisaidii kuwafanya marafiki zako waweke simu chini, basi hakuna kitakachoweza kuwazuia.

Ulimwengu halisia

Tunapenda intaneti– kuna mengi sana ya kujifunza na kufanya na kufikiria juu ya intaneti. Unapoishiwa na mambo ya kurambaza kwenye Google, kuna zile picha za kuchekesha za paka!

Usisahau yale yaliyo muhimu hasa: ambao ni watu walio karibu nawe. Marafiki zako. Familia yako. Wale unaowajali. Hakikisha upo katika maisha yako ili uwe na mambo ya 'kupenda' na 'kushiriki' katika ulimwengu ulio halisia.

Share your feedback