Jinsi Kusaidia Wengine Kulivyonisaidia Kujiamini
Jambo! Jina langu ni Sophia, nina umri wa miaka 14 na ninaishi na mama yangu na nyanya yangu katika mji mtulivu ambao hakuna chochote ambacho hutendeka. Kwa bahati mbaya, usiku mmoja, jambo mbaya lilitendeka. Madarasa mawili shule ya mtaani kwetu yaliungua. Kwa bahati nzuri, hakuna aliyeumia, lakini wanafunzi wa darasa la nne na la tano walilazimika kuanza kusomea nje.
Mimi huenda kwa nyanya yangu kila Jumapili. Sio jambo ninalopenda sana duniani, lakini huwa linalipa kitu cha kufanya, haswa wakati wa likizo. Siku moja, jirani yake alituambia kwamba kampuni kubwa la ujenzi kutoka jijini lilikuwa limesikia kuhusu madhara yale kwenye redio na likatoa vifaa vya kuyajenga tena. Sasa, kijiji kilihitaji watu wa kujitolea kusaidia kujenga madarasa yale.
Nilipatwa huruma sana juu ya wanafunzi wale na nilitaka kusaidia. Lakini kwa kweli, nilikuwa na woga sana kuhusu kujitolea kwa sababu mimi sio bora kwa mambo mengi na sifahamu chochote kuhusu ujenzi! Lakini niliamua kujaribu, kwani nilikuwa na muda mwingi wa ziada wakati wa likizo.
Waliniweka kwenye timu ya usimamizi na kazi yetu ilikuwa kuhakikisha kwamba vifaa tulivyokuwa navyo vilitumiwa vizuri nai wale wanaojitolea. Tungekuwa kwenye shida kubwa sana kama saruji ingeisha kabla ya madarasa yale kukamilika! Kila siku nilitakiwa kuandika idadi ya vifaa tulivyowapa wanaojitolea na kiasi gani kilibakia. Lilikuwa jukumu kubwa na mwanzoni nilikosea. Lakini nilivumilia na nikazidi kuwa makini na kwa muda nikawa bora katika hilo.
Ilituchukua muda wa wikendi nne kumaliza majengo yale na mwishowe nilijivunia sana. Katika kutafakari, niligundua siku zote nimekuwa bora katika kupanga mambo. Kwa mfano, mama yangu siku zote hunifanya nipange vyakula vya maadhimisho ya sikukuu. Hata hivyo, kwa kusaidia watu wengine, nilikuja kugundua kwamba nilikuwa bora kwa jambo fulani! Kwa nini usijaribu? Huwezi jua kwa kiasi gani kujitolea kutakusaidia kugundua talanta fiche!
Kwangu, kugundua talanta fiche inayowasaidia watu wengine kulinifanya kugundua kwamba mimi ni muhimu na ninapaswa kujiamini na kuamini uwezo wangu. Hata bora zaidi – imenifanya kuwa jasiri zaidi hata kujaribu mambo mengine mapya!
Share your feedback