Kuwa mjanja

DIY inapiku vya madukani kwa kila namna.

Kwa nini ukinunue ilhali unaweza kukitengeneza? Huweki tu akiba ya pesa nyingi kwa kuunda vitu vyako, bali pia ni duka bora la ubunifu. Na kwa mapana, ni bora zaidi kuunda kitu kipya kutokana na nyenzo zilizopo kuliko kununua vitu zaidi. Bado unapata msukumo? Tuanze: 1. Msukumo uko kila mahali
Katika enzi hii ya intaneti, unaweza kupata msukumo zaidi kuliko awali bila kuondoka nyumbani. Tatizo ni misukumo kupita kiasi. Utaanzia wapi unapotaka kuwa msanii? Tembelea tovuti kama Pinterest au Etsy, ambapo wasanii wengi wa nyumbani na waundaji wanaonyesha kazi zao. Tafuta ‘DIY’ au ‘mawazo ya sanaa’ na voila! Utapata duni mya yenye mambo. Je, siku ya kuzaliwa ya rafiki yako wa dhati itakuwa wikendi hii? Usiharibu pesa ukinunua vitu ghali! Badala yake mpe vifaa au vito vya nywele ambavyo ulijitengenezea. Atafurahia kabisa kwa sababu imetoka kwenye moyo wako na ni ya kipekee, kama urafiki wenu!

2. Tumia ulicho nacho
Una habari kuhusu kitu cha kutengeneza lakini huna uhakika cha kutengenezea? Angalia ulipo. Kutengeneza vitu si lazima kutumia nyenzo mpya kabisa, kuwa mbunifu na urekebishe vitu ulivyo navyo nyumbani. (Hakikisha kuwa hakuna mtu mwingine anayetumia vifa hivyo kwanza!) Wazo la kukufanya kuanza: geuza shati la zamani kuwa mkoba mpya, pata maagizo hapa.

3. Jipange
Vitu viko kwenye chumba chako? Usiviache kuendelea kurundika, vikusanye na uvipange ili msukumo unapokuwepo, uwe utayari. Ukweli: watu kwa kawaida hutumia takribani saa 38 kwa mwaka kutafuta vitu vilivyopotea. Huenda unatumia wakati huo kuunda vitu vipya maridadi. Hivyo tu! Hakuna sheria zilizowekwa za DIY au kuunda, ingia tu na uanze kutengeneza kitu! Na inaleta raha sana kutengeneza vitu na marafiki, kwa nini usikusanye marafiki zako wikendi hii kwenye karamu ya sanaa?

Share your feedback