Kufahamu msingi wa jambo

Jieleze msichana!

Hujambo! Ndiyo, wewe! Kwa masikio na macho! Umewahi kuchushwa? Kuwa na msongo wa mawazo? Kuhuzunika? Kumpenda mtu? Kuvunjwa moyo? Umewahi kushangaa jambo la kufanya kutokana na hisia nyingi na za ajabu na nzuri zaidi? Tuna jibu:

SANAA!

Usijali ikiwa unafikiria kuwa wewe si msanii — sanaa ni chochote unachotaka kuwa, na sanaa ni ya kila mtu! Sanaa ni kitu chochote kinachoelezea hisia na mawazo ya mwanzilishi wake na kuunda mhemko kutoka kwa watu wanaoithamini. Unapopenda maneno ya wimbo? Sanaa! Au maandishi yanalandana na ulichokuwa ukihisi moyoni mwako? Sanaa!

Sanaa ya Kuishi, Kuishi Sanaa
Jambo bora kuhusu sanaa ni kuwa inakuundia uwezekano usio na kipimo ili kujieleza duniani. Unahisi kuchushwa na kutopata msukumo? Densi! Densi ni mwondoko na vitendo, lakini pia inaweza kuwa njia ya kujieleza kikamilifu. Cheza densi na marafiki, au peke yako chumbani.

Ikiwa umo katika sanaa za kuona, ni rahisi kama kuchukua karatasi na kalamu. Hakuna hukumu, ufungue moyo wako kabisa. Chora mambo yote yaliyo akilini mwako. Usijali ikiwa mtu anakupa majibu hasi; jifunze kutokana na maoni ambayo unadhani ni muhimu na upuuze mengine yote.

Au wewe ni mwandishi? Labda unaishi kwa kusimulia hadithi na kuandika. Baadhi ya wasanii maarufu walikuwa waandishi! Soma Chimamanda Ngozi Adichie na Hoda Barakat na utazame maneno yako yakicheza densi kwenye ukurasa. Na ikiwa una marafiki waliosoma makala mengi, unaweza hata kuunda kilabu chako binafsi cha vitabu. Uandishi mzuri na marafiki wazuri huandamana.

Kujifunza kuthamini sanaa kunamaanisha kujifunza kuthamini mengi zaidi maishani. Ndiyo, sayansi, sheria, hisabati, na uhandisi ni muhimu zaidi. Bila shaka ni muhimu. Lakini nyimbo, upakaji rangi, michoro, fasihi, densi — hivi ndivyo vitu tunavyovifanya maishani. Bila sanaa, maisha yetu yasingekuwa na rangi, au muziki, au drama.

Kwa nyakati zote maishani mwako, za furaha na huzuni, sanaa inaweza kukupa jibu. Unachohitaji kufanya tu ni kujieleza.

Share your feedback