Wasichana wanaweza kufanya hilo!

Kutana na wasichana watano wa ajabu wanaleta tofauti.

Leo, wasichana wengi wanatimiza mambo ambayo watu wengi walifikiri yasingwezekana. Kutana na wasichana watano ambao wameonyesha ulimwengu kuwa hakuna kitu ambacho msichana hawezi kufanya!

Laura Dekker kutoka Uholanzi ni mtu mchanga zaidi kuendesha mashua kote ulimwenguni... mwenyewe! Kwanza alihitaji kuishawishi serikali yake kumruhusu ajaribu na kuwapiga vita watungaji sheria ambao walijaribu kumzuia. Lakini alisimama imara na kushinda. Laura alikamilisha safari yake ya miaka miwili mnamo Julai 2012 akiwa na umri wa miaka 16. Mikaila Ulmer alianzisha biashara yake, Me & the Bees Lemonade, alipokuwa tu na miaka minne. Kinywaji maarufu kimetengenezwa kutoka kwenye juisi ya limau, maji na asali. Baada ya kushambuliwa na nyuki mara mbili Mikaila aliamua kujifunza yote ambayo angeweza kuhusu nyuki wa asali na kugundua jinsi walivyo muhimu kwa asili. Sasa kila chupa ya kinywaji cha limau anayouza inatoa hela za kuwatunza nyuki hawa.

Eva Tolage alimwandikia barua Barack Obama, Rais wa Marekani, alipokuwa na umri wa miaka 14. Ndani yake alitaka hatua zaidi kuchukuliwa ili kupambana na umaskini katika kijiji chake nchini Tanzania na kote ulimwenguni. Barua yake pia ilizungumza kuhusu jinsi yeye na wasichana wengine walivyokabiliwa na njaa na ukosefu wa elimu, maji safi na umeme. Barua ya Eva iliwahamasisha viongozi ulimwenguni kuchukua hatua kwenye Umoja wa Mataifa.

Niloofar Rahmani ni rubani wa kwanza wa kike kufunzwa katika jeshi la Afghani. Yeye na familia yake walikabiliwa na vitisho vingi lakini alivumilia ili kukamilisha mafunzo yake. Mwaka wa 2015, alituzwa Tuzo ya Wanawake Jasiri kwa ushujaa wake.

Judi Lerumbe kutoka Kenya alikuwa tu na miaka 15 baba yake alipojaribu kumlazimisha kuolewa na mwanamume mzee. Kwa usaidizi kutoka kwa mama wa kambo, Judi alitoroka kijiji chake na kujiunga na Umoja, kijiji salama cha wanawake pekee ambapo wasichana wanaweza kuenda shuleni badala ya kuolewa wakiwa wachanga. Leo Judi anafanya kazi katika makavazi yanayosaidia kuvutia watalii kwenye eneo lake na kuunda ajira kwa wanawake wa karibu.

Share your feedback