Fuata hatua hizi tatu rahisi
Sisi sote tumepitia hili – uko darasani na huelewi somo, lakini una aibu sana kuzungumza. Mtu mwingine ananyanyua mkono juu na kuuliza swali lile lile rahisi ulilokuwa na aibu kuuliza na ghafla kila mtu anakubali kwamba anahitaji usaidizi pia. Au pengine mnajiburudisha na marafiki na umemuona mtu unayemtamani. Unachotaka ni kwenda na kuzungumza naye, lakini hauna ujasiri wa kutosha. Msichana mwingine anapoanza kuzungumza naye unagundua kwamba ni mcheshi na mwenye urafiki na unawaza, “Ningeweza kufanya hivi.”
Hapa kuna hatua tatu za kukusaidia kuondoa aibu, uzungumze na uwe huyo mtu jasiri unayetaka kuwa!
Jiamini. Sura zinaweza zikadanganya, kwa hiyo hata kama hauna ujasiri, ukionekana na utende kwa hatua fulani, utashangaa jinsi inavyosaidia kubadilisha mtazamo wako.
Usijali sana! Maisha ni yamejaa vigingi vigumu na ukiuliza maswali ya upuzi au umpoteze rafiki kwa sababu ya jambo mnalotofautiana au kujiaibisha mbele ya mtu unayemtamani, unapaswa kujipa moyo tu na uendelee na maisha. Itakufanya kuwa mtu hodari.
Jiamini. Hata kama unaona aibu sana kuzungumza, unajua unachokifanya, kwa hiyo anza kuamini ujuzi na maarifa yako. Kadiri unavyojiamini, ndivyo unavyokuwa jasiri.
Sasa nenda ujaribu mbinu hizi na punde utaanza kujihisi jasiri zaidi, ndani na nje.
Share your feedback