Malengo ya uhusiano - Mmi na mama

Fahamu jinsi uhusiano wako na mama unavyofana!

Kina mama!

O-M-G, M-O-M.

Kina mama! Hatujui kinachoendelea na kina mama lakini kila mara wanapata njia ya kuvuruga siku yetu. Huwa na matarajio makubwa ya ajabu na kanuni na kazi na vitu vya kutatiza maisha yako na huuliza kila mara kwa nini huwezi kuwa kama dada yako. Hukasirika kuhusu kitu!

Ni vipi mtu huyu aliyeniumba awe akinisumbua hivi?!

Baridi, uso wa msichana. Hili hapa ni funzo unalohitaji ambalo hakuna anayekuambia unapokua: shughulikia uhusiano wako na Mama yako. Huenda si mkamilifu, lakini hakuna aliye mkamilifu — na hilo linakujumuisha! Mwisho wa siku, mna miaka mingi ya pamoja na nyote wawili mtahitajiana.

Tuache mchezo na kutafuta suluhisho.

Chukua hatua ya kwanza.
Jumapili hii, pangeni ziara ya sokoni na mpike pamoja baadaye. Au, unafahamu kile ambacho anafurahia kufanya. Mwonyeshe mama yako kwamba hata ingawa wakati mwingine nyote wawili mnapaziana sauti, bado unaelewa kuwa yatapita. Si kazi yake tu kukutunza, ni kazi yako kumtunza. Kuenda matembezi nje na kufanya jambo kunarahisisha kuzungumza kuhusu kinachokuudhi.

Mtu ambaye anakuelewa kabisa Bla, bla, wasiwasi wa kijana, unahisi kuwa mgeni, kusubiri kumpata mtu anayekuelewa kabisa, bla bla. Wewe na msichana mrembo zaidi daima. Unamtaka mtu ambaye labda ataelewa jinsi unavyohisi? Mjaribu mama yako. Kila kitu unachopitia, tayari ameshapitia. Acha mchezo na uzungumze na mama yako kuhusu kinachokuudhi.

Kusema ‘samahani’ ni rahisi Sawa, wakati mwingine kunatokea vita kati yako na wazazi wako ambavyo si vitu vidogo — ni vitu vikubwa vinavyobadilisha maisha. Hatuzungumzii kuhusu vitu hivyo.

Tunazungumzia wakati huo mmoja ambao uliwaona marafiki zako ulipoenda na mama yako kufanya ununuzi, na ukampazia sauti kwa kukuaibisha mbele yao. Tunazungumzia mambo ya kuudhi. Mambo ambayo unapoyafikiria, unajua lilikuwa kosa lako.

Unapofanya mambo ya kuudhi, omba msamaha. Sehemu ya kukua ni ya kuwajibika unafanya makosa. Huenda akaonekana kama aliyeumbwa kwa jiwe, lakini mama hukwazika pia. Kujifunza kusema samahani kunaweza kuleta tofauti kubwa sana, na ni stadi itakayokusaidia maishani mwako mote.

Share your feedback