Unahitaji zaidi!
Unajua kwamba akili yako ni kama uwanja wa kivita. Ni kawaida kuwa na mawazo mazuri na mabaya yanayopingana. Yote yanapigania umakini wako. Wakati mwingine unaweza kuhisi ni kama mawazo mabaya yanashinda, lakini haipaswi kuwa hivyo wakati wote. Katika kila vita kuna mikakati ya kushinda na hata wewe uko vile - MSHINDI.
Basi hebu tuanze kazi, ili uweze kujifunza jinsi ya kuepuka mawazo mabaya na kuacha kuwa mchoyo kwako mwenyewe. Je! Mko tayari kufanya kazi fulani, Wana Springster? Vizuri Chukua penseli na kitabu.
Hatua ya 1 - Weka mambo katika mtazamo
Tunaporuhusu mawazo mabaya kuzingatia mawazo yetu, kwa kawaida tunasahau mambo mengine yote ya ajabu yanayotuhusu. Hivyo kila wakati wazo baya linapotokea tunahitaji kufundisha akili zetu kufikiria jambo moja zuri mara moja. Andika katika kitabu chako jinsi ulivyogeuza wazo baya kwa mfano hakuna mtu anayenipenda kuwa wazo nzuri kwa mfano Mimi ni mtu mwenye upendo na mwenye kujali, na watu hunipenda jinsi nilivyo.
Hatua ya 2 - Unajionaje mwenyewe?
Unakuwa kile unachoamini. Hivyo ikiwa unaamini huwezi kufikia malengo yako, kuna uwezekano mkubwa hutaweza kuyafikia. Badala yake, amini mambo mazuri kujihusu. Kuwa na maneno ya kusema ambayo unaweza kurudia kila asubuhi. Kwa mfano unaweza kusema:
MIMI NI WA THAMANI
NINA NGUVU
NINA KUSUDI
Andika chini mara 100 ikiwa inafaa na kusema kwa sauti ya juu zaidi ili ulimwengu usikie!
Hatua ya 3 - Sahau yaliyopita
Ni ajabu jinsi ambavyo kumbukumbu za makosa zinahifadhiwa kwa karibu ndani ya akili zetu lakini kumbukumbu nzuri zinahifadhiwa kwa umbali sana? Ikiwa unatumia wakati wako wote kuwaza makosa yako basi huwezi kujiamini sana. Kwa hiyo, kwenye kitabu chako, andika jambo uliloshindwa au kosa moja na chini yake andika kile ulichojifunza kutoka kwa kosa hilo. Kuzingatia kile ulichojifunza badala ya kosa ulilofanya kutakuongeza hekima na furaha maishani!
Hutapata mtazamo mzuri mara moja lakini unaweza kuchagua kuwa mkarimu kwako mwenyewe kila siku na kukumbuka mambo mazuri kuhusu wewe mwenyewe.
Share your feedback