Unatendewa vibaya?

Una haki

  • Katika nchi nyingi wanawake na wasichana wana haki sawa kama wanaume kwa mujibu wa sheria, na wanachukuliwa kuwa sawa katika hali zote. Lakini hili halifanyiki nyumbani kila mara.
  • Una haki ya kuheshimiwa na kuwa salama nyumbani kwako. Iwapo hali si hii basi zungumza na mtu unayemwamini kama mwalimu au kiongozi wa kijiji. Tatizo linaloshirikiwa linaweza kuwa mzigo ulioondolewa.
  • Iwapo mtu mzee zaidi anajaribu kukutisha kwa kukupigia kelele au kukuumiza, inaweza kuwa dhuluma na ni makosa. Tafuta mtu mzima unayemwamini akusaidie.
  • Mtoto huwa na kiwewe zaidi anapompoteza mzazi wake kuliko kitu kingine. Kukua bila wazazi au mtu mzima wa kukutunza kunaweza kumaanisha uko katika hatari zaidi ya madhara. Lakini bado una haki ya kupata elimu na huduma ya afya.

Share your feedback