Kuwa Mwenye Afya, Kuwa na Furaha

Ishi maisha yenye afya na furaha

Ninafahamu jinsi unavyohisi kuambiwa mimi ni mnene. Niamini.

Nina tumbo kubwa sana na furaha ya marafiki zangu huongezeka pindi tu wanapoliona tumbo langu likiwa kubwa kuliko matiti yangu ninapovaa shatitao linalobana. Unapaswa kuridhika ulivyo haijalishi una uzani kiasi gani, lakini hebu tuseme ukweli: huwa si jambo rahisi.

Wakati fulani hata nilifikiria kumeza tembe zangu za lishe, lakini baada ya kutafuta kwenye intaneti kuhusu madhara yake, nilibadilisha nia yangu mara moja. Sio tu kwamba si nzuri kiafya, bali tembe nyingi za lishe unazoweza kupata hapa hazijasajiliwa na mdhibiti wa afya!

Baada ya kufahamu madhara ya kumeza tembe za lishe, nimeanza kufahamu kuhusu jinsi ya kupoteza uzani wangu kwa njia ya kiasili. Mama wa rafiki yangu wa dhati ni daktari na nilimwomba ushauri kuhusu jambo hili. Alinipa vidokezo vya lishe bora kwa vijana kama sisi.

1. Weka Lengo
Lengo dogo linaweza kuwa mwanzo mzuri wa kupoteza uzani wako. Kwa mfano, ikiwa unapenda kula vyakula vilivyokaangwa, unaweza kuweka lengo la kupunguza kuvila.

2. Kunywa maji mengi
Daktari Mita alisema kuwa ninahitaji kunywa angalau bilauri 8 za maji kwa siku. Kunywa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupoteza maji na pia yanapunguza uzani wako, kwa sababu yanajaza matumbo yetu, na kuturahisishia kushiba tunapokula.

3. Shiriki katika Michezo na Uhakikishe kuwa Umeuchezesha Mwili Wako Sana
Kukimbia, kutembea kwa kasi, au mazoezi ya densi ni mfano mzuri wa michezo inayoweza kupunguza uzani wako. Pia, ukiwa kwenye jumba la biashara, jaribu kutumia vidato badala ya kambarau. Kupanda au kushuka vidato kunaweza kuangamiza kalori nyingi sana kwenye mwili wako haraka zaidi.

4. Kula Ufumwele Mwingi
Ufumwele ni mzuri sana kwa mwili wetu, unaweza kufanya mfumo wetu wa umeng`enyaji kuwa wa afya, kupunguza mafuta yetu na pia uzani wetu. Jaribu kula ndizi, brokoli, tufaa na mboga za majani.

5. Badilisha Kabohaidreti kwa Kabohaidreti Ngumu
Wali, tambi na mkate ni vyanzo vya kabohaidreti, lakini inabainika kuwa vyakula hivi ni vigumu kumeng`enya. Pia inawezakujaza mafuta, kwa hivyo ni vyema tukitumia kabohaidreti ngumu yenye kiwango cha juu cha ufumwele kama uji wa shayiri, wali wa hudhurungi, viazi, au mahindi.

6. Epuka Vyakula vya Haraka
Vyakula vya haraka au vilivyofungwa vina kiwango cha juu cha kalori na mafuta, bila kusahau vihifadhi na ladha. Hizo ndizo sababu unapaswa kujaribu kuepuka vyakua vya haraka.

Ninajua si jambo rahisi kupoteza uzani kwa njia zilizotajwa hapo juu, si rahisi kama kumeza tembe za lishe, lakini kila kitu kina utaratibu. Afya yako ni muhimu zaidi kuliko kila kitu, na vitu vizuri haviji kwa urahisi, sivyo?

Share your feedback