Urembo huwa wa kila rangi

Muhimu ni kile kilicho ndani

Tunasikia kila mara: tuna ngozi ya maji ya kunde na wasichana ‘warembo’ wana ngozi nzuri. Watangazaji wangependa uamini kuwa ngozi yetu nyeusi hairidhishi – na kwamba wana suluhisho ambalo ni sabuni za kubadilisha rangi ya ngozi na mafuta na dawa za kutibu.

Wakati umefika wa kutambua kuwa ngozi zote ni maridadi. Unaweza kusema kuwa Lupita Nyong’o, Sasha na Malia Obama, au Prianka Chopra si warembo? La! Wasichana hawa wana mafanikio na ni warembo — na wote wana ngozi ya maji ya kunde! Ni warembo kwa sababu wana ujasiri na wanajithamini zaidi kuliko sura zao.

Maana ya urembo si ngozi nzuri, nywele ndefu iliyonyoka, na mwili mwembamba pekee. Watu wengi sana wenye aina tofauti za mili, hali ya nywele, vitu usoni, na rangi za ngozi huwa warembo. Kinachowafanya kuvutia ni ujasiri wao!

Kuna mambo mengi yasiyofaa kwa desturi ya kuwafanya wasichana waamini kuwa ngozi yao si sahihi, lakini hebu tuanze kwa lile rahisi: bidhaa nyingi si hata salama!

Watengenezaji wasiojali hutumia kemikali na viungo hatari kwa bidhaa za kubadilisha ngozi kuwa nyeupe, kama steroidi, hidrokwinoni, na zebaki. Vitu hivi vinaweza kudhuru sana na vinaweza kusababisha matatizo mengi sana ya ngozi, ikiwemo kovu la milele, sumu ya zebaki na kifo! Inatisha!

Bidhaa nyingine za kubadilisha ngozi kuwa nyeupe hutumia maneno yanayotia moyo, kama “mitishamba” na “asili,” ili kukufanya uamini kuwa ni salama. Ukweli ni kuwa, vitu vingi ni vya kiasili, lakini hilo halimaanishi kuwa ni vizuri kwako: hata baadhi ya kemikali hatari duniani zinaweza kupatikana katika asili — nyingi zenye sumu zinaweza kuitwa asili, lakini bila shaka hatutaki kujipaka kwenye nyuso zetu!

Rangi ya ngozi yako ina urembo jinsi tu ilivyo, na ukiwa jasiri na mwenye furaha, unasambaza hata kitu kizuri zaidi kuliko ngozi nzuri: unang`aa kwa urembo wa ndani!

Share your feedback