Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi!
Enyi wote! Mimi ni Saliha! Ninapitia kitu fulani, jambo ambalo si kawaida kushirikisha watu wengine, lakini ninawaamini ninyi wasichana hapa, hivyo ...
Hivi karibuni mwili wangu umekuwa ukibadilika. Kwa halisi, Matiti yangu. Yanakuwa!
Sikuwa na uhakika kama hiyo ilimaanisha nilikuwa napitia kipindi cha kubalehe.
Kwa hiyo nikamwuliza mama yangu, naye akajibu kwa faraja, "Mpennzi wangu, hiyo inamaanisha kwamba unakua, sasa wewe ni kijana. Homoni zako zinaanza kufanya kazi, na wakati huo, matiti yako yataanza kukua. Unaweza kusikia aina ya maumivu na ukakasi karibu na eneo hilo, lakini hiyo ni ya kawaida. Mara baada ya kuanza hatua hiyo, matiti yako yataanza kukua, ikimaanisha unahitaji kuanza kuanza kuvaa sindiria! "
Mama alifafanua kwamba kila msichana hupitia hali hii. Na ni mwanzo tu. Baadaye nywele zitaota kwenye makwapa yako na kuzunguka uke wako, umbo la mwili wako hubadilika na kisha hedhi huanza.
Mama aliniambia kuwa kati ya umri wa miaka 8-13, matiti yetu yataanza kukua polepole. Baadaye, kati ya miaka 12-14, tunaweza kuona maumivu juu au kuzunguka chuchu, tunaweza pia kusikia uvimbe chini yake. Uvimbe huo huitwa kichomozo cha matiti na unaweza kuwa mdogo kama buluuberi au kubwa kidogo. Katika kipindi hiki, wasichana wanaweza kuanza kuvaa sindiria ndogo.
Pia, wakati wa hedhi, tunaweza kusikia maumivu kwenye matiti yetu, na hilo pia ni jambo la kawaida!
Kama alama za vidole vyetu, matiti yetu ni ya upekee na binafsi kama sisi, yanakuja katika kila maumbo na ukubwa wa aina tofauti. Kila msichana ni wa kipekee. Wa kipekee, kiasi kwamba ukubwa wa kulia na wa kushoto unaweza kuwa tofauti, baadhi ni makubwa na mengine ni madogo, na hii ni kawaida pia.
Usizingatie lolote juu ya kile unachokiona kwenye televisheni kuhusu umbo bora la mwili wa mwanamke. Sisi ni tofauti na tunapaswa kujivunia hilo!
Unalohitaji kujua ni, wasichana wote vijana watalazimika kupitia kipindi cha kubalehe. Wasichana wengine watapitia mapema zaidi kuliko wengine, wengine huenda wakapitia kwa kuchelewa. Usiogope ikiwa unajisikia matiti yako bado hayajaumbika ... Na kwa wale ambao wameshafanikiwa, usihangaike ikiwa yamekuwa makubwa kama milima au vilima, jambo muhimu ni tunakua na afya njema! Kwa sababu sisi sote tumekamilika kwa upekee wa kila mmoja wetu wenyewe!
Share your feedback