Maboyz na Wadada

Hawana tofauti sana!

Jina langu ni Anna, nina miaka 16. Mimi ni wa kwanza katika familia yetu, na nina ndugu mapacha, Jenny na Jimmy, ambao wana miaka 12.

Baada ya Jenny kufika miaka 12, mwili wake ulianza kubadilika haraka na akaanza kujiona mkubwa kuliko kaka yake pacha Jimmy. Jenny akaanza kuhisi tofauti katika mwili wake. Alikuja kwangu na kunielezea. Nilimwambia amefika kipindi kinachoitwa ubalehe. Na kila mtu katika darasa lake shuleni pia atapitia hili. Vijana wadogo wanakuwa wakaka wakubwa na wasichana wanakuwa wadada kamili. Lakini akasema kuwa haoni kama Jimmy anabadilika. Nikamweleza kuwa pia Jimmy atabadilika, ni vile tu wakati mwingi wasichana hufika ubalehe mapema.

Wiki kadhaa baadaye, jirani wetu Benny akakuja kucheza na kina Jenny na Jimmy. Benny akasema tayari ameshaanza kuona mabadiliko. Nikaona dadangu ameanza kuridhika kuona Benny pia alikuwa anapitia jambo sawa na yeye. Wakaanza kuongea vile miili yao imebadilika ndani na nje. Wakagundua kuna mabadiliko yanayolingana kama kurefuka na kuongeza uzito. Na pia kuna mabadiliko hayafanani kama vile Jenny kupata hedhi kila mwenzi na Benny kuota ndoto nyevu anapolala.

Wote wawili walikuwa wanajiuliza maswali mengi na hawakuwa wanajua cha kufanya wakati huo wa ubalehe. Wakaniuliza wanastahili kufanya nini. Na mimi kama rafiki yao na dada mkubwa nikawashauri, ”Kuwa tu vile uko!”

Nafurahi kuwa Jenny aliongea na mimi kuhusu mabadiliko ambayo mwili wake ulikuwa unapitia na nilikuwa tayari kumsaidia ili aweze kutulia na kuwa tayari kuona mabadiliko zaidi, kufurahia ubalehe wake, gupata taarifa sahihi kuhusiana na mwili wake. Na sasa anamsaidia pacha mwenzake Jimmy kujitayarisha kuona mabadiliko pia.

Ni kawaida sana kuongea na wengine kuhusu mabadiliko kwenye mwili wako, iwe marafiki, wazazi au mtu ambaye tayari amepitia ubalehe. Hakikisha umemtafuta mtu ambaye huna shida kuongea naye.

Hapa nina dokezo; tulia unapoongea, eleza maswali yako vizuri, kisha hakikisha unasikiliza kwa makini mawaidha ya mshauri wako.

Share your feedback