Tuna majibu!
Dadangu mpendwa,
Nilikuwa nikiongea na rafiki yangu. Nikamweleza vile tulikiss na mvulana fulani. Lakini yeye alisema hiyo inamaanisha nimefanya ngono. Ni kweli?
Hebu nieleze!
Lota_girl100
Hi Lota_girl100,
Asante kwa swali lako!
Ikifika ni ngono watu husema mambo tofauti na ni mada inayochanganya. Hivyo usijali, hauko peke yako. Tunashukuru ulituma ujumbe huu kwa Dada zako WanaSpringster ili kujua ukweli.
Unaweza kuwa umesikia mambo tofauti kuhusu ngono. Watu wengi husema kuwa ngono ni wakati uume (ogani ya mapenzi ya mwanamume) inapoingia ndani ya uke (ogani ya mapenzi ya mwanamke). Lakini hilo si ukweli, ni zaidi ya hilo.
Hebu tuangalie kwa undani pindi ngono ilipomaanisha kufanya mapenzi. Ukitizama hivi, ngono ni mwili mmoja kugusana na mwigine na wote wawili kusikia vizuri na kila mmoja anashiriki.
Kwanza, cha muhimu ni kuwa kila mtu anafaa kuamua ikiwa anataka bila kulazimishwa. Kama wote wako sawa, basi ngono yaweza fanyika iwe mko na nguo ama mko uchi.
Unasemaje? Ngono mkiwa mmevaa nguo? Ndio. Ngono huku mkiwa mmevaa nguo inawezekana. Kukiss, kushika matiti, miili kugusana yanaweza kufanyika mkiwa mmevaa nguo. Na kama unaskia raha, na unafikiri hii ni ngono, basi ni ngono.
Inapofika ngona bila nguo, kuna viwango tofauti. Kuna kukiss, kushika au kulamba sehemu za siri, na pia kuna kuingia ndani ya uke au mkundu. Kuingia ni pale mtu mmoja anaingiza sehemu ya mwili wake ndani ya mwili wa mtu mwingine.
Watu hufanya ngono ionekane jambo kubwa, lakini ni jambo la kawaida sana. Wakati mwingine unaeza kushiriki ngono na kuskia poa, na wakati mwingine usikie uchungu. Unaweza kuhisi tofauti ukishafanya ngono, hivyo hakikisha uko tayari kabla ya kuanza sfari hii.
Hivyo maana ya ngono inaweza kuwa tofauti na jinsi ulivyodhani, lakini unapaswa kujua mambo 2 MUHIMU SANA ya kuzingatia kabla ya kushiriki ngono:
Natumai hii imekuwa ya manufaa kwako!
P.S. Kamwe usisahau: Mwili wako. Chaguo lako.
Share your feedback