Vidokezo na mbinu rahisi
Maisha yamejaa juu chini na ubalehe unapokuja, unaweza kusikika kama chini zaidi kuliko juu.
Mwili wako unapitia mabadiliko mengi sana unapobalehe, kihisia na kimwili. Ni mengi kukabiliana nayo, lakini ni vyema kujua ya kutarajia na kukumbuka kwamba inatendeka kwetu sote.
Wasichana wataanza kupata matiti na wanaweza kuanza hedhi. Wavulana watavunja sauti na kuwa nzito. Nywele itaanza kumea kwenye makwapa na sehemu za siri. Homoni hizi zote zikibadilika mwilini wako, unaweza kupata mhemko wa hisia na chunusi.
Kwa kweli, chunusi ni chungu - inahisi kama kila mtu anaangalia madoa makubwa mekundu usoni mwako. Lakini usiwache zikuweke chini. Hazitakuwa hapo milele na unaweza kujaribu tiba kuu ya asili kusaidia ngozi yako...
1. Kunywa maji mengi
Kuna faida nyingi kwa kunywa maji mengi. Mwili wako umetengenezwa na 70% maji, kwa hivyo kukunywa maji ya kutosha kunaboresha digestive system, inayosaidia kutoa sumu na kuhakikisha mwili wako unatoa rutuba zinazohitajika kwenye ngozi yako. Matokeo ni wazi, ngozi inayong’aa.
2. Jaribu kifuniko cha uso kinachoponya
Kifuniko cha uso cha asali na dalasini ni mbinu bora ya kiasili kuzuia ngozi yako isiharibike. Zote zina sifa za kuzuia uvimbe na kupambana na bakteria. Changanya vijiko viwili vikubwa vya asali na kimoja cha dalasini kutengeneza paste. Paka mchanganyiko huu usoni mwako baada ya kuosha na iwache kwa dakika 10-15 kabla ya kuoga. Fanya hivi mara moja kwa wiki.
3. Punguza mafadhaiko
Ni ngumu kumaliza mafadhaiko kabisa (kazi za nyumbani, wavulana, ndugu wasumbufu) lakini unaweza kudhibiti kwa kupata usingizi wa kutosha, kufanya yoga au kutafakari, mazoezi na kuvuta pumzi mara kadhaa. Unapokuwa na mafadhaiko machache, ngozi yako inapata furaha!
Jaribu suluhu hizi rahisi na utaona matokeo. Kama hakuna kinachoonekana kufanya kazi, zungumza na mtu mzima unayeamini atakayekupa ushauri zaidi na kukuhakikishia kwamba haitadumu milele.
Oh na kumbuka... Ukiwa na chunusi au bila, wewe bado ni mrembo!!
Share your feedback