Masomo yanayohusu kujipenda mwenyewe kutoka kwa rafiki yangu wa dhati
Njia 5 zilizonisaidia kuupenda mwili wangu zaidi
Mambo Springsters
Nina jambo la kuungama.
Kila wakati nilipojiangalia kwenye kioo wakati wote niligusa sehemu zilizonenepa au nilitoboa chunusi fulani usoni. Ndani yangu mlikuwa na sauti inayosema mmi sikuwa mzuri. Katika kukua kwangu niliteswa shuleni na watu walipachika majina mabaya sana hivyo nikaona vigumu kujiamini
Sikufurahia kulalamikia hali ya mwili wangu, lakini ilikuwa vigumu kwangu kujipenda wakati sikupenda kile nilichokiona kwenye kioo.
Wiki mbili zilizopita nilipokuwa natembea kwenda nyumbani kutoka shuleni na rafiki yangu wa dhati Selen, nilifunguka nikamwambia jinsi niliyotamani kuupenda mwili wangu na kujipenda zaidi. Alinipa ushauri mzuri sana ambao uliniwezesha kuhisi vizuri mara moja.
Haya ndiyo niliyofunzwa na rafiki yangu wa dhati kuhusu kujipenda mwenyewe. Natumai ushauri huu utakusaidia kama ulivyonisaidia mimi.
- Mara tu unapokuwa karibu kujitoa makosa mwenyewe, acha kufanya hivyo na ujisemee, *je, ninaweza kumfanyia hivyo rafiki yangu?* Jibu yamkini ni la. Wewe ni rafiki wa wewe mwenyewe kwa hiyo jitendee ukarimu.
- Unapojiangalia kwenye kioo, zoesha akili yako kutazama yale mambo mazuri unayopenda na si yale mapungufu unayoyachukia. {Kwa hiyo sema maneno kama haya, *Ninaweza kutopenda miguu yangu lakini nina sura ya kupendeza na macho mazuri sana.*
- Tambua kuwa uzito wako na ukubwa wa rinda lako si muhimu. Thamani yako haitegemei uzani wa mwili wako. Una mengi mazuri koliko kilo zako kwenye mizani. Wewe ni nafsi nzuri sana, u mwerevu na mwenye lengo. Usiache wasiwasi huu uwe kizuizi cha ukuu wako.
- Acha kuolinganisha mwili wako na miili ya marafiki zako. Marafiki holeta thamani kubwa katika maisha yako. Ni muhimu kutumia muda kufurahia kuwa pamoja nao na kurusha roho koliko kujilinganisha. Sisi sote ni wa kipekee na tunapendeza sana!
- Unaweza kuwa mwenye afya njema ukiwa na uzito wowote. Kukonda hakumaanishi utaishi miaka mingi. Afya yako ndicho kitu muhimu zaidi. Kwa hiyo weka malengo ya kuwa na afya njema badala ya “kuonekana mwembamba”. Fanya mazoezi mara kwa mara na ole lishe bora- hiyo ndiyo siri ya kuishi maisha marefu!
Nawashukuru sana marafiki zangu kama Selen. Sasa ninaupenda mwili wangu na ninawafundisha wasichana wengine waipende miili yao pia.
Share your feedback