Tuzungumzie hedhi

Ni wakati wa kukomesha unyanyapaa.

Ama alikuwa akienda nyumbani kutoka mjini siku moja, alipopata hedhi yake. Alihisi mgonjwa na mchovu lakini alipoona watu wakitembea na kumpita, aliona ukweli:

"Kila mtu anayepita dunia hii alianza kama yai na kisha mimba," alitafakari. "Mwili wangu - mwili wa kila mwanamke - hupitia hali hii * ili jamii ya mwanadamu iweze kuwepo*. Kwa nini hatuzungumzii jambo hili? "

Uchovu wa kutozungumza
Ama aliamua kufanya jambo. Shuleni, alimwambia rafiki yake wa dhati wazo lake - wanapaswa kuwauliza wasichana darasani ikiwa wanataka kukutana baada ya muda wa masomo ili washirikishane wasiwasi waliyonayo.

Hiyo ndivyo ilivyoanza klabu ya Power Period (Nguvu ya Hedhi). Baada ya kukutana, wasichana walihisi kuwa wa kawaida na kutokuwa wapweke.

Mwenye hekima na afya njema
Kadiri wasichana walivyokutana, walihisi wenye nguvu zaidi - kama timu. Haya ni baadhi ya mambo waliyojifunza pamoja:

Kuanza hedhi yako haimaanishi wewe 'uko tayari' kufanya ngono. Msichana mmoja alikiri kwamba alikuwa na hofu hedhi yake ingemaanisha amekuwa mwanamke na lazima awe tayari kwa ajili ya ndoa na kuzaa watoto. Wakati marafiki zake waliposema mwili wake ulikuwa tu 'katika mazoezi', kwamba ilikuwa ni kawaida kujisikia kuwa hakuwa tayari kwa ajili ya 'marathon', alijisikia vizuri.

Maumivu ya kuungua wakati unakojoa sio sehemu ya kawaida ya kupata hedhi yako. Msichana mmoja katika kikundi alipoanza kutumia visodo, alianza kutaka kukojoa mara nyingi zaidi, na alisikia kuungua wakati anakojoa. Alidhani ni kisodo kilikuwa kinagandamiza sehemu zake za ndani. Lakini wasichana wengine walisema haikuwa ikitokea kwao. Alizungumza na mama yake, ambaye alimtuma kliniki. Alikuwa na maambukizi ya kibofu - cystitis. Wanawake wengi hupata maambukizi haya, lakini katika hali kali, inaweza kuenea mpaka kwenye figo zako ikiwa haitatibiwa.

Homoni zinaweza kuyumbisha kujiamini kwako - lakini unaweza kuwa tayari kuzikabili. Wasichana wachache katika kikundi walisema walijisikia kufadhaika wakati wa hedhi zao. Waligundua kwamba walijihisi kuwa dhaifu, wasiopendeza au wenye huzuni kwa sababu ya kile kilichokuwa kinatokea katika miili yao, si kwa sababu ya uhalisia wao. Walikubaliana kuwa na kujijali wenyewe na kwa kila mmoja katika wakati huo.

Faragha si sawa na siri. Wasichana walidhani watu walichukulia hedhi kwa namna fulani kama chafu kuliko vitu vingine vitokavyo mwilini kama jasho, kamasi na kinyesi. Watu wanahisi faragha kuhusu miili yao lakini wanaamua kuwa si sawa na kuwa msiri au kuwa na aibu. Kwao ilikuwa muhimu kushirikishana, kwa sababu kuweka mambo kuwa siri kunaweza kuwa na madhara.

Kumbuka, ikiwa unataka kuanzisha kikundi chako, vitu unavyosikia - au kusoma - si vya kweli wakati wote. Unapotafuta majibu - hususan mtandaoni - hakikisha kwamba yanatoka kwenye chanzo unachokiamini.

Share your feedback