Chat za hedhi - na wavulana !

MUNGU WANGU!

Naitwa Aisha. Nina miaka 16 na naishi na baba na kakangu. Mama alifariki nikiwa mdogo.

Nikiwa na miaka 11, niligundua damu kwenye chupi. Hili likanichanganya. Sikujua damu imetoka wapi, na sikujua kilichokuwa kinaendelea. Nikachukua nguo nzee, nikairarua na kuitumia kuzuia damu.

Nilijifunza kutoka kwa wasichana wengine shuleni kwamba nilikuwa nimeanza hedhi zangu. Nilikuwa na maswali mengi lakini sikujua nitazungumza na nani!

Lakini siku moja nikasoma kwenye Springster vile unaweza kuongea na baba yako kuhusu hedhi. Nikajikakamua na nikaongea na baba. Mwanzo hakutaka tuongee, alidhani mimi bado mtoto. Lakini nilipomwarifu kuwa tayari nimeanza hedhi zangu, akaitikia kuongea.

Aliniambia yote kuhusu hedhi! Wasichana wanazaliwa na maelfu ya mayai, mirija miwili ya kupeleka mayai kwenye tumbo la uzazi, na tumbo moja la uzazi. Tumbo hili la uzazi lina nguvu ya kushikilia mtoto hadi kuzaliwa.

Msichana anapoanza kubalehe, yai moja ndogo sana linatoka kwenye ovari na kuelekea katika tumbo la uzazi. Wakati huo, damu na tishu zinaanza kuwekwa kwenye kuta za tumbo la uzazi, ili kufanya kuta hizi kuwa nene ili kutayarisha tumbo la uzazi ikiwa mwanamke atapata mimba.

Ikiwa hakuna mimba, tumbo linaondoa tishu ya ziada, damu, tishu na yai ambalo halijatungwa. Shughuli hii ya kuondoa ndiyo inayojulikana kama hedhi. Hii hutokea kila mwezi - isipokuwa wakati mwanamke ni mjamzito, au kwa sababu nyingine, kama vile ishu za lishe au hata stress.

Miezi michache baadaye tulijadili hedhi kama mada katika darasa. Wavulana walitaka kujua zaidi. Niliwaeleza kwa ujasiri. Wasichana wengine waliona aibu, lakini nikawashauri wasione aibu kuzungumza juu ya hedhi - ni kawaida na ishara kwamba unakua mwanamke.

Share your feedback