Njia za kuhisi vizuri hata unapohisi vibaya zaidi
Tunajua kuwa maumivu ya hedhi yanaweza kuwa ya kutisha. Mwili wako huuma, unahisi kuchoka zaidi, na sehemu zako za ndani kuhisi unyong`onyevu na kukosa raha. Jambo baya zaidi ni kuwa hali hii ni ya kila mwezi.
Msichana anapaswa kufanya nini?! Unapaswa kuteseka? Au kumeza tembe ili kuondoa maumivu na ukosaji raha? La! Hizi hapa ni njia rahisi na za asili za kukufanya kuhisi vyema na kuwa mwenye afya wakati huo wa mwezi.
Kula vyema:
Matunda na mboga ni bora kwa ajili ya kuridhisha kiu chako cha sukari na makali yoyote ya njaa ya ghafla. Hata bora zaidi? Ni vizuri kwako! Vina vitamini na ufumwele ambavyo mwili wako unahitaji ili kuendelea kuwa imara na wenye afya. Pia vinaongeza nishati yako na ni njia bora zaidi ya kupata sukari ya ghafla kuliko chokoleti! Bora zaidi ni kuwa, ni rahisi kupata matunda na mboga freshi. Huenda kwa sasa una bakuli lililojaa vitu hivyo jikoni mwako!
Dumisha usafi
Tunapopata hedhi zetu, tezi zetu za joto na za sebashia hufanya kazi mara mbili. Kuoga kwa maji moto kutaondoa joto na mafuta ya ziada kwenye ngozi yako na kutuliza neva, na hata kupunguza maumivu ya hedhi. Hakikisha kuwa umeosha uso wako kabla ya kulala pia - ngozi yenye mafuta mengi husababisha kuwepo kwa vidudusi!
Unapopata hedhi, sehemu zako za siri zinaweza kuwa nyeti sana na unyevunyevu wa ziada unaweza kusababisha uvamizi wa kuvu na bakteria. Ili kuepuka maambukizi yenye mwasho, osha sehemu hiyo taratibu (sehemu ya nje pekee – usiingie ndani!) kwa maji safi na sabuni kidogo, kisha ugongegonge kwa taulo safi.
Hakikisha kuwa u safi, unabadilisha kitambaa cha hedhi kila mara unavyopaswa – takribani kila baada ya saa tatu au nne ni muda wa kawaida.
Na mwisho: tunafahamu si rahisi kila wakati kuwa msichana, hivyo kuwa mzuri kwa wasichana walio karibu nawe! Kwa pamoja, tunaweza kufaulu kwa jambo lolote!
Share your feedback