Hedhi….kipi cha kawaida?

Na kipi sio cha kawaida?

Mawazo yako (1)

Kupata hedhi yako kuna maana zaidi ya kutokwa damu kila mwezi kuwa sehemu ya maisha yako. Homoni zako huweka ovari na tumbo lako kufanya kazi, na huenda ukahisi hisia zako zinazulika pia. Huu 'mzunguko wa kila mwezi' unaweza kuchukua kati ya siku 21 na 40. Hapa kuna baadhi ya ukweli kukusaidia kuhisi umeelimika na kuwa tayari!

Mayai yanaweza kukufanya upate kichefuchefu

Baadhi ya wasichana wengine wanaweza kuhisi wakati wao wa kutokeza yai, karibia katikati ya mzunguko wao. Unaweza kuhisi kichefuchefu kidogo na maumivu madogo sehemu ya chini mgongo au tumbo. Unaweza hata kuhisi mlipuko kidogo au mngurumo wakati yai linatoka!

Kuuma mtindo wako
Ni kawaida kupata maumivu au 'mkazo' wakati wa kutokwa hedhi. Ukuta wa tumbo lako hukaza kusaidia ukuta mwembamba kutoka. Wasichana wengine hawahisi hali hii, wengine huhisi maumivu ya kuvuta, baadhi hupata mawimbi ya maumivu. Ikiwa ndio unaanza, maumivu ya tumbo yanaweza kuwa mabaya mara ya kwanza, lakini hupungua baada ya muda.

Moto, kuumwa, kupwita, kuwa na chunusi na madoa, kukosa furaha!
Unahisi kama hedhi yakarahisha? Hauko peke yako. Mzunguko wako unadhibitiwa na homoni - estrojeni kuwezesha mayai yako kusafirishwa, projestroni kuandaa tumbo lako. Inaweza ikatisha hisia zako. Ni kawaida kuhisi hasira, mwenye kilio kingi na mkali kabla ya hedhi yako, kupata maumivu mgongoni au ukakasi katika matiti, chunusi na kupwita. Kula vizuri, mazoezi ya taratibu, kutumia dawa za kupunguza maumivu na kuoga maji ya moto vinaweza kusaidia.

chupi chini ya uchunguzi
Kila msichana ni tofauti linapokuja swala la kinachotoka kwenye chupi zao - lakini maji ya uke au 'utoko' ni ya kawaida. Yanawezekana kuwa meupe au ya rangi ya krimu katikati ya mzunguko, au unaweza kupata madoa ya rangi ya kahawia kabla au baada ya hedhi yako (ni damu tu iliyochanganyika na oksijeni). Sio kitu cha kuonea aibu, wala cha kuogopesha.

Wakati wa kumuona muuguzi au daktari

  • Ikiwa una maumivu makali wakati unapoangua au kutokwa damu.
  • Kama unatokwa damu nyingi sana (kama vijiko 3-5 ni kawaida kwa kila hedhi).
  • Ikiwa unapata madoa ya kahawia kwa zaidi ya siku chache.
  • Ikiwa unapata vidonda karibu na uke wako, utoko mzito, unaotoa harufu isiyo ya kawaida, wa kijani, njano au kijivu - haya yanaweza kuwa ishara ya maambukizi hivyo uwe na ujasiri na ukapimwe.

Share your feedback

Mawazo yako

Njoki

Na kama unatoa hyo uchafu unakaa mweupe kila siku shinda n ipi

Machi 2, 2024, 3:12 p.m