Wasichana wanapozungumza wenyewe...

Mambo ya ajabu hutokea!

Ninapowasili nyumbani kutoka shuleni, kitu ninachopenda kufanya ni kusubiri kuanza kwa programu ya Saa ya Nguvu ya Msichana katika ya redio. Ni wakati maalum ambapo watangazaji wanazungumzia kuhusu masuala maalum yanayoathiri wanawake na wasichana wadogo kama mimi na wewe.

Wiki iliyopita watangazaji walikuwa wakizungumzia kuhusu mwonekano wa mwili. Kulingana na watangazaji, mwonekano wa mwili ni mojawapo ya wasiwasi mkubwa kwa wanawake vijana. Uchunguzi wa mtaa uliofanywa ulibaini kuwa msichana 1 kati ya 3 aliacha kupendezwa na mwonekano wa mwili wake alipofika ubalehe. Wengine walihisi hawakupendeza vya kutosha, na wengi walihisi si wembamba vya kutosha. Hili hutokea kwa sababu wasichana wengi hawafahamu jinsi ya kushughulikia mabadiliko yanayotokana na ubalehe na kuzeeka.

Hili lilinishangaza sana! Mamangu aliniambia kuwa napendeza na mimi ni wa ajabu jinsi nilivyo, lakini nadhani wengi wa wasichana hawakuungwa mkono kwa namna hii. Nilitaka sana kufanya jambo kuhusu hili, hivyo niliwaalika marafiki zangu chumbani kwangu baada ya shule ili kuzungumzia suala hili.

Tuliketi pamoja na kushiriki hisia na maoni yetu kuhusu jinsi ilivyo kuwa wanawake vijana wanaokua huku wamezungukwa na picha za miili ambayo ni tofauti na yao. Kuzungumza kuhusu mabadiliko tuliyopitia wakati wa ubalehe ulinidhihirishia jinsi hadithi zetu zote zilivyolingana. Wasichana waliohisi upweke hapo mbeleni wakatambua kuwa sio wao tu waliopitia uhusiano wa kupenda-kuchukia miili yao. Angalia hapa dada, huko peke yako katika yale unayopitia. Kuzungumza na marafiki waaminifu kuhusu mwili wako na mabadiliko unayopitia hukufunya kupata nguvu hata zaidi.

Baada ya kuzungumzia mambo haya, tuliamua kutafuta suluhu. Tulizungumzia njia mwafaka za kupenda zaidi miili yetu. Hatimaye tuliahidiana kwamba tutakoma kulinganisha miili yetu na watu wengine. Miili yetu hubadilika kwa njia tofauti na za kipekee na kwa sababu sisi sote tunapitia ubalehe, hiyo ni hali ya kawaida kabisa.

Mazungumzo haya ya baada shule sasa yamegeuka na kuwa klabu imara ya wasichana ambapo tunazingatia mazungumzo muhimu kuhusiana na ubalehe na mambo tunayopitia kama wasichana! Nilianza na wasichana 5 na sasa nina 50!

Tunapozungumza pamoja kama wasichana, tunafundishana na kujifunza kutoka kwa kila mmoja na HAKUNA chochote cha nguvu zaidi kushinda hicho.

Share your feedback