Dorcus alizaliwa na kukulia Nakuru Kenya na kuhamia Nairobi. Ilibidi afanye mtihani wa Cheti cha Masomo ya Msingi ya Kenya (KCPE) wakati wa mgogoro wa 2007 katika eneo lao. Wakati huu, alilazimika kuhama ambao kulimsababisha apambane kupata ada ya shule hadi mama yake alilazimika kuuza kitanda chake ili kutumiza mahitaji ya familia. Hii haikukatisha tamaa ya Dorcus, aliweza kuingia chuo kikuu na kupata kazi. Mara tu baada ya hayo, mawazo yake ya kujitolea na kuwa na juhudi kulimsaidia kuanzisha kampuni yake ambapo hutoa huduma kama Kocha wa Uongozi, Mkufunzi wa Kampuni, na msemaji wa Hotuba Msingi/Kutoa Motisha.
Dorcus alitumia matukio ya maisha yake kuwasaidia wengine kupambana na hali ngumu - alitumia changamoto zake zote na akazibadilisha kuwa mafundisho ya kumsaidia kuendesha maisha yake na kitu chochote kinachoweza kumpata.
Kwa kifupi, angependa kuwaonyesha wasichana kuwa haijalishi unatoka wapi, umepitia nini na umezaliwa kwa familia gani. Kitu ambacho unahitaji pekee ni “kujiamini na vitendo vinavyohitajika kusonga mbele”.
Mambo 5 ya kweli kukuhusu: Ninawajibika, ninajaribu kila wakati kufanya mambo ifaavyo, nimejipanga, mimi ni mbunifu na rafiki.
Ulikuwa na matarajio/malengo gani ukikua? Nilitaka kufanya kazi katika tasnia ya kifedha na kupata digrii ya usimamizi wa biashara. Nilitaka pia kuhakikisha kuwa ninaweza kusaidia familia yangu kupata chochote wanachohitaji.
Watu walitoa maoni mabaya ulipowaeleza kuhusu malengo yako? Eh, ndiyo!Mtu fulani alinielezea kuwa wasichana hawapaswi kuelimishwa. Hii ilinipa motisha wa kujitahidi zaidi kwa sababu, nilijua jiinsi kukaa shuleni kungenifaidi.
Kidokezo cha elimu cha #GirlPossible Shule inaweza kuwa ngumu, na tunaelewa kuwa unataka tu kuendelea, kisha uanze maisha yako. Lakini kama Dorcus, elimu haina thamani, itakusaidia kufanya maamuzi siku moja na itakupa chaguo kadhaa za kuchagua wakati utakapofika. Inaweza kukusaidia kufungua uwezo wako kamili.
Ulishughulikia aje maoni yasiyofaa? Nilijaribu kuwa na mtazamo mzuri kila wakati. Nilijiamini na nikapata vitu vya kunitia motisha. Nilisheherekea mwenyewe kwa kukumbuka ninachoweza kufanya na nilijitahidi kufikia malengo yangu.
Ulipewa ushauri gani bora wa kutekeleza malengo yako? Niliambiwa nijitahidi kufikia malengo yangu.
Ushauri gani bora ambao umewahi kuambiwa? Nifanye kazi kama punda nikiwa shuleni na kuishi kama mfalme/malkia siku za usoni AU niishi kama mfalme/malkia nikiwa shuleni na nifanye kazi kama punda siku za usoni.
Ni mambo gani 4 ambayo yaliyokusaidia kulenga ndoto zako? 1. Niliandika malengo yangu yote na kujisomea, mara kwa mara. 2. Nilijiona nikifanikisha malengo yangu. 3. Nilitafuta maelezo ya kile ninachohitaji ili kuanzisha biashara yangu mwenyewe.
Ulijiambia nini ulipotaka kukata tamaa? Nilijikumbusha kwamba kuendelea kusoma kutanifaidi katika siku za usoni. Pia nilijikumbusha kuhusu mambo ambayo wazazi wangu walijitolea kufanya ili niweze kwenda shuleni na kufanikiwa.
Kwanini unafikiri ni muhimu kuweka malengo? Malengo hukusaidia kutembea katika njia inayofaa unapojitahidi kufanikisha ndoto zako. Siku zote huwa unakumbuka kama wimbo. Kuweka malengo kunaweza kukusaidia kupambana na nyakati ngumu unapovunjika moyo.
Kidokezo cha #GirlPossible cha kuweka malengo Kwa Dorcus, sio lengo moja tu ambalo lilimfanya aendelee. Hatua ndogo zilimsaidia kufikia ndoto kubwa. Kuwa msemaji wa kutoa motisha, ilibidi asiogope kuzungumza mbele ya watu wengine, lengo ndogo ambalo lilimsaidia kuanzisha kila kitu. - Ainisha malengo yako - Panga hatua yako ya kwanza - Usiogope kutofaulu.
Kidokezo cha #GirlPossible cha kuzungumza kuhusu malengo yako Dorcus alikuwa anakabiliwa na mambo mengi mabaya kuhusu kutaka kuwa mfanyabiashara na kuanzisha kampuni yake mwenyewe. Lakini alitegemea familia yake na marafiki wa karibu, watu ambao aliwaamini. Kumbuka: ● Anza kwa kuzungumza na watu wanaokujua na unaowaamini ● Tafuta watu katika jamii yako ambao wameanzisha biashara zao wenyewe au wanaoweza kusaidia kuendesha biashara, ndogo au kubwa. Wanaweza kukupa maelezo ya kile unapaswa kufanya ili kuanzisha biashara yako mwenyewe. ● Anza na marafiki wako wa karibu na utafute njia yako. Familia, marafiki, wamiliki wa biashara – hawa watakusaidia kujiandaa kwa ajili ya mazungumzo ya baadaye.
Una ujumbe mgani kwa wasichana kama wewe? Fikiria kwa umakini kuhusu malengo yako na uyaandike. Tafuta kile unahitaji kufanya kuyafikia. Kwa mfano unapaswa kusoma nini na unahitaji masomo gani? Kaza fikra na ujiamini. Usisikilize watu ambao wanasema kuwa huwezi kuifanya.
Ni wewe pekee unayeelewa jinsi kufikia ndoto zako ni muhimu kwako. Haijalishi unatoka wapi, unapitia nini sasa au ndoto zako ni kubwa kiasi gani. Unaweza. Jiamini na uwezo ambao unayo.
Kupata #GirlPossible yako Inaweza kuhisi ni kama inachukua milele kufikia lengo hilo lakini kumbuka kuwa hatua unazoweka zinakusaidia kujiandaa. Kwa Dorcus kazi yake haikuanza haraka, lakini alijua thamani ya elimu. Unataka kujua aje? ● Saa hizo zote katika darasa la hesabu humsaidia sasa kusawazisha vitabu vyake. Hesabu = pesa! ● Kulazimika kufanya maonyesho mbele ya darasa huenda kulitisha mara ya kwanza, lakini hakujua kuwa hiyo ilikuwa anamuandaa kwa ajili ya siku zake za usoni za kuwatia motisha watu wengine kama yeye. ● Kupata kazi ya kumsaidia kulipia shule kulimfundisha jinsi ya kuwajibika.
Fikiria jinsi elimu yako inavyokusaidia kujiandaa kwa ajili ya maisha yako ya baadaye.
Share your feedback