Mahitaji dhidi ya vitu vya ziada – tofauti ni nini?

Catherine anapenda nguo. Hivi majuzi aliona nguo ambayo amekuwa akiiwazia kwa miezi mingi.Kwa bahati mbaya, bei yake ni ghali mno. Kutokana na bajeti yako ndogo, ilimbidi Catherine abaini iwapo nguo ilikuwa hitaji au kitu cha ziada.

“Ninapenda mitindo kila wakati. Tatizo ni kwamba sina pesa kila wakati za kununua vitu vyote vya kupendeza ninavyotaka. Ninamaanisha kuwa ninavyohitaji. Au sivyo? Ni vigumu kubaini tofauti!”

Unapofiriki kuhusu vitu ambavyo tunavihitaji mara nyingi hutokana na vitu ambavyo hutufanya tuwe na afya (kama vile chakula) na salama (kama vile makazi). Fikiria kuhusu vitu unavyohitaji wakati wa hedhi yako au sabuni na dawa ya mswaki; vyote hivi hutufanya tuwe wenye afya. Hata vitu kama vile sare za shule ni kitu cha muhimu kukipa kipaumbele.

“Ninapofiriki kuhusu mahitaji haya, ninagundua kuwa ninafahamu kuwa manufaa ya vitu hivi vyote ni ya kudumu kwa muda mrefu kuliko nguo; vitanisaidia si tu siku baada ya siku lakini pia katika maisha yangu ya baadaye” anasema Catherine. “Vinaweza kunisaidia kujitayarisha katika kukabiliana na changamoto zozote ambazo huenda nikakumbana nazo… lakini… bado nawazia kuhusu nguo! Kwa hivyo, hiyo inamaanisha nini? Nimegundua kuwa nitakuwa na vitu vya ziada kila wakati, lakini ninapaswa kuyapa mahitaji yangu kipaumbele na pia kupangia maisha ya baadaye. Kupangia maisha ya baadaye na vitu ambavyo huenda nitahitaji - na vya ziada - inamaanisha kutengeneza mpango wa kuweka akiba!”

Catherine aliketi na kutengeneza mpango wa kuweka akiba kwa kutumia hatua hizi 4:

1. Fikiria kuhusu maisha ya baadaye: kupata na kutumia pesa

Sasa Catherine alielewa kuhusu mahitaji yake, aligundua vitu kadhaa ambavyo angevipa kipaumbele cha kununua kwa kutumia mapato yake kutokana na kazi ya kutunza watoto. Iwapo alitaka kununua zaidi ya vitu hivi (kama vile nguo!), Catherine alihitaji kutengeneza mpango wa kutengeneza pesa zaidi. Aliamua kuhusu kuoka vitafunio vya kupeleka shuleni na kuviuza wakati wa chakula cha mchana. Hatua hii ingeongeza mapato yake na kumaanisha kuwa angeweza kuweka akiba.

2. Weka akiba mara kwa mara (hata kama ni kiasi kidogo tu)

Sasa Catherine alielewa kikamilifu kiasi ambacho angepeta kila mwezi kutokana na kazi zake na alikuwa amefanya hesabu kuhusu gharama ya vitu vyake vyote vyenye umuhimu, alifahamu kikamilifu kiasi ambacho angesalia nacho ili kuweka akiba kila siku. Katika baadhi ya miezi hakuwa na muda wa kuoka au kuwa na muda mwingi dukani, lakini, bila kujali kiasi kidogo alichokipata, alihakikisha kuwa alitenga kiasi fulani cha pesa ili kuweka akiba mara kwa mara.

3. Weka akiba mahali salama

Kwa sababu Catherine hana akaunti ya benki, alitaka kuhakikisha kuwa aliweka pesa zake kwa njia salama. Alihitaji mahali salama, pasipotambulika kwa urahisi na pengine kwa mtu anayemwamini ambaye angeweza kumtegemea. Mwishowe, Catherine alimwomba shangazi yake kumwekea akiba yake kwa njia salama. Hatua hii pia ilihakikisha kuwa asingepeta majaribu ya kutumia pesa!

4. Shughulikia upungufu katika kuweka akiba

Mapungufu ni ya kawaida, kwa hiyo, Catherine alijaribu kuweka rekodi ya mambo yoyote yanayoweza kutokea yasiyotabirika kama vile kuwa mgonjwa na kutoweza kutunza watoto. Alijua kutovunjwa moyo kwa kuwa wakati mwingine ni vigumu kufuata mpango au kufanikisha malengo yetu, iwapo tutafuata mpango wetu, utatusaidia.

“Unajua nini? Baada ya miezi minne nitaweka akiba ya pesa za kutosha ili kupata nguo hiyo! Na pia nimeweza kuwashauri marafiki zangu kuhusu kuweka akiba. Ninajivunia zaidi kufuata mpango wangu wa kuweka akiba!”

Share your feedback