Mashambulio, risasi….hutendeka hapa

Azimio la Msichana linasema: Kataa dhuluma!

Tulipounda Azimio la Msichana, zaidi ya wasichana wachanga 500 walihojiwa kwenye nchi zote 14. Kisa cha Andressa kinaakisi changamoto zinazowakabili wasichana wengi tuliozungumza nao...

Dhuluma dhidi ya wanawake na wasichana

Kama wasichana wengi waliochangia kwenye Azimio la Msichana Andressa mwenye umri wa miaka 16 kutoka Brazil alizungumzia hatari za dhuluma anazokabiliwa nazo kama msichana. "Mashambulio, risasi," anasema. "Sitadanganya kuwa mambo mengi hutendeka hapa."

Ndiyo sababu lengo la 3 la Azimio linahusu kuhakikisha usalama wa wasichana, ili waishi bila woga wa dhuluma na unyanyasaji.

Andressa pia anazungumzia dhamira yake ya kupata elimu ili ayaboreshe maisha yake na ya familia yake. Dhamira hiyo iliungwa mkono na wasichana wote waliohojiwa, ambayo ndiyo sababu ya lengo la 2 la Azimio kuangazia kuimarisha uwezo wa wasichana kuenda shuleni na elimu bora wanayopata.

Share your feedback