Niliaibika shuleni

Kujifunza kudhibiti hedhi zangu

Mawazo yako (1)

Wasichana kote duniani kwa kawaida hupata hedhi kati ya miaka 12 - 14, lakini wanaweza kuzipata mapema au baadaye. Kupata hedhi zako kunaweza kushangaza au kuogopesha. Hiki ni kisa cha msichana mmoja.

Jina langu ni Deepa. Nina miaka 13 na ninaishi India. Nilipata hedhi zangu mwezi uliopita. Nilipoona damu kwenye chupi (underwear) yangu nilishangaa, lakini sikuogopa kwa sababu mama yangu aliniambia kuwa ningeanza kupata hedhi zangu muda fulani nikiwa na miaka 12.

Niliiosha chupi yangu na kumwambia mama yangu kilichotendeka. Alifurahi sana kwa kuwa binti yake alikuwa amehitimu kuwa mwanamke! Alinipa kifurushi cha sodo (sanitary pads) na kunionyesha namna ya kuvalia kwenye chupi yangu. Lilikuwa jambo geni kwangu lakini nilikuwa SAWA kwa wiki nzima.

Mwezi mmoja baadaye, nilirejea shuleni. Ilianza kama siku ya kawaida hadi nilipoanza kuhisi hali tofauti tumboni mwangu. Nilihisi kama niliyekuwa na maumivu. Nilidhani nilikuwa mgonjwa na sikujua kuwa ilikuwa dalili ya kupata hedhi zangu. Nilipata hedhi siku hiyo na sikuwa tayari.

Ilinibidi kuondoka shuleni mchana kwa sababu sketi yangu na kiti changu vilikuwa na damu. Nilidhani kuwa lazima kila mtu awe ameiona. Niliaibika sana. Sikutaka kurejea shuleni tena.

Nilipofika nyumbani mama yangu alinikalisha chini na kuniambia kitendo kama hiki kilimtokea dada yangu. Alisema tunaweza kuhakikisha kuwa hakitatokea tena kwa sababu ninaweza kufuatilia hedhi zangu na kujua wakati wa kuzipata mwezi unaofuata, kwa kuwa hedhi zangu huja karibu kila baada ya siku 28.

Alisema, "Unaweza kuvuja damu kwa siku 5 mwanzoni mwa kila mzunguko. Mzunguko wa hedhi huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya hedhi yako hadi siku ya kwanza ya hedhi nyingine. Kwa wanawake wengi mzunguko wa hedhi ni kati ya siku 21 hadi 35. Tutatia alama kwenye kalenda yako"

Nilirejea shuleni siku iliyofuata na hakuna aliyesema chochote kuhusu kisa hicho. Hakuna aliyetambua wala kujali. Lilikuwa funzo gumu la kujifunza kwangu, lakini ninashukuru mama yangu, kwa kalenda na taarifa.

Share your feedback

Mawazo yako

Brian

Hello?

Sep. 30, 2022, 8:18 p.m