Kupata imani ya kujieleza

Jinsi hatua ya kuomba msaada ilivyobadilisha kila kitu

Nilipokuwa ninakua kuwa mtu mzima nyumbani mwetu, nilikuwa msichana pekee miongoni mwa wavulana watatu, sikuwahi kusikika vya kutosha. Zaidi ya hayo, nilimsaidia mamangu kuwatunza babu na bibi yetu. Sikuwa na furaha kweli kwa kuwa nilkuwa na mambo mengi ya kufanya na sikuwa na muda wa kujihudumia lakini sikutaka kukasirisha familia yangu. Muda wowote wa ziada niliokuwa nao, nilisoma vitabu vya ndugu yangu mkubwa na kupitia maisha ya wahusika tofauti.

Mambo yalianza wakati Mwalimu wangu wa Kiingereza alipoanzisha Klabu ya Kusoma Vitabu shuleni. Nilijua litakuwa jambo ambalo lingenipendeza, kupata fursa ya kusoma hata zaidi lakini nilikuwa na uoga wa kuomba muda wa ziada ili kuhudhuria. Nilianza kukata tamaa kwa kuwa sikutaka kuhisi kuwa haya ndiyo maisha yangu yote. Licha ya kuwa jambo la kuogofya, nilijua kuwa ninapaswa kujaribu kujieleza.

Nilifikiria kuwa njia bora zaidi ya kuweza kuwaelezea wazazi wangu ni kuwa na mtu ambaye angenipa ujasiri na ushauri. Ndugu yangu mkubwa ndiye ambaye ninahusiana naye kwa ukaribu zaidi katika familia yangu. Huwa tunazungumzia kuhusu vitabu ambavyo yeye hunipa na kufanya mzaha kuhusu hadithi ambazo tungependa kuandika siku moja. Niliamua kumweleza kuhusu kutaka kuwa na muda zaidi wa ziada. Alinipa baadhi ya ushauri ambao nitaukumbuka kila wakati:

  1. Tayarisha yale unayotaka kuzungumza mapema na utoe mifano yako ambayo inaunga mkono hoja yako.
  2. Chagua muda na mahali ambapo kila mtu ametolia na anafuraha. Hatua ya kuzungumza ukiwa na haraka hufanya iwe vigumu kuwa na mazungumzo yanayofaa.
  3. Jua kuwa furaha yangu iko mikononi mwangu. Hata iwe vigumu vipi kujieleza, ni muhimu kujieleza.
  4. Kuwa na yeye kama mshirika wangu ilimaanisha kuwa sikuwa pekee yangu.

Mazungumzo yake yalinisaidia kweli. Wakati mamangu aliporudi kutoka kazini, nilimketisha chini na kumweleze hisia zangu. Alisema kuwa hakutambua kuwa nilijihisi kulemewa na alikasirika kuwa sikuona kwamba ningeshiriki naye hisia zangu mapema. Tulikubalina kuwa ni jambo nzuri kwangu kuenda kwenye klabu ya kusoma ila niahidi kuwa muwazi zaidi kwake siku za baadaye. Ninafuraha zaidi kuwa ndugu yangu alinihimiza kwa kuwa sasa ninahisi kuwa na uwezo wa kujieleza siku za baadaye.

Je, kuna mtu ambaye amekuhimiza kujieleza? Tuambie katika sehemu ya maoni

Share your feedback