Safari yangu ya kujipenda na kupenda sauti yangu
Ninajiita “malkia wa mitandao ya kijamii” kwa sababu ninapenda kuchapisha kuhusu maisha yangu na motisha yangu kwenye mitandao ya kijamii. Lengo langu ni kupenda mwili na ninalenga kusambaza imani na uwezeshaji kupitia machapisho yangu. Kutokana na hayo, jumuiya ya kupendeza imekua kati yangu na wanaonifuatilia.
Watu hushangazwa kila wakati kusikia kuwa sikuwa hivi wakati wote, ilinichukua muda kujenga imani yangu na kujihisi huru katika ngozi yangu.
Nilipoanza kuwa mtu mzima, kujiangalia kwenye kioo lilikuwa jambo gumu zaidi na ningejaribu na kuepuka kujiangalia kadri nilivyoweza. Nilipowasha Runinga au kuangalia mitandao ya kijamii, niliona wanawake warembo na laini ambao walipaswa kusherehekewa na kila nilipokuwa shuleni, wasichana ambao walionekana kama wanawake waliokuwa kwenye Runinga ndio ambao walizungumziwa zaidi.
Imani yangu ilipungua kwa kasi zaidi na nilijaribu kukaa mbali na Runinga na mitandao ya kijamii ili kujizuia kujilinganisha na kuwa na wasiwasi kuhusu jinsi ninavyofanana.
Miaka kadhaa iliyopita, nilijiunga na shule ya uanahabari jambo ambalo lilinipa furaha zaidi mwalimu wangu aliponishauri ili kuwa bora katika darasa lake. Nilihitaji kuwa katika mitandao kijamii ili kujifahamisha kuhusu matukio ya ulimwenguni na kuelewa jinsi uanahabari ulivyokuwa ukibadilika.
Nilikuwa na wasiwasi kuhusu kujaribu na nilimweleze wasiwasi wangu lakini alisema atanisaidia kupambana na hali hiyo. Nilifungua baadhi ya akaunti mchana huo na maisha yangu yakabadilika baada ya muda mfupi.
Nilitambua kuwa kwa kutumia mitandao ya kijamii ningeweza kudhibiti sehemu ya mambo niliyokuwa ninasoma na kuona. Kutoka kwenye mipangilio ya faragha hadi kutofuata vituo vyenye maudhui hasi, nilitengeneza maudhui yangu mwenyewe. Mhadhiri wangu pia alinihimiza kuwa mtu wa kuleta mabadiliko niliyotaka kuona mtandaoni, “Tumia mtandao wako wa kijamii kubadilisha ujumbe ambao unafikiri kuwa hauwafai wasichana wadogo,” alisema.
Nilianza kutumia Instagram na ukurasa wangu wa Facebook kuchapisha hadithi za kutia motisha kuhusu mambo niliyoyaona katika mazingira yangu - hasa katika kupenda mwili wako na wanawake walionivutia. Kurasa zangu zilihusu kuwa huru katika mwili wako na nilianza kugundua kuwa wasichana wengi walikuwa wakifuata kurasa zangu. Walitaka kuona hadithi kuhusu jinsi ya kufuata maisha ya afya yenye furaha kadri nilivyofanya! Kupitia mitandao ya kijamii, niliweza kuzungumza, kuanzisha vuguvugu kuhusu kujipenda mwenyewe na kuanzisha jumuiya ambayo inasherehekea wanawake na mambo tunayoyathamini zaidi.
Je, unaweza kujipenda kwa njia gani? Je, unaweza kufanya mambo gani ili kusherehekea urembo wako? Tuambie kwenye maoni hapa chini
Share your feedback