Jinsi mimi na rafiki yangu Lesedi tulivyoanzisha klabu ya mjadala

Tulisaidiana

Mimi na rafiki yangu Lesedi tunapenda kusoma vitabu na kutazama mijadala kwenye runinga. Tungetumia masaa mengi kujadili kuhusu mada tofauti kama vile - kila kitu kuanzia kwa iwapo masomo ya chuo kikuu yanapaswa kuwa ya bila malipo au iwapo mashindano ya urembo yanapaswa kupigwa marufuku.

Mmoja wa walimu wetu Bw. Nkosi alitusikia tukizungumza kuhusu kipindi cha mjadala ambacho sisi hutazama kila wakati, The Big Debate, na akapendekeza kuwa tuanzishe klabu yetu sisi wenyewe ya mjadala.

Tulitengeneza machapisho ili kuweka shuleni kote na baada ya muda mfupi neno likasambaa na tukapata watu 15!

Mwanzoni, nilikuwa na wasiwasi kuhusu kushiriki maoni yangu kwa kikundi lakini kadri wiki zilivyopita na nikajifunza jinsi ya kutoa hoja yenye uzito, imani yangu ilijengeka na niliweza kuwasaidia wengine kushinda aibu zao.

Tuligundua mada nyingi zaidi na tuliweza kufikiria kuhusu mambo kutoka katika mitazamo tofauti pamoja na kujifunza jinsi ya kuzungumza hadharani. Si tu kwamba ninajihisi kuwa na uwezo wa kujieleza na kutoa maoni yangu sasa, lakini ninaburudika sana kila wiki.

Je ungependa kutengeneza klabu yako mwenyewe ya mjadala? Hivi hapa ni vidokezo maarufu:

1. Chagua baadhi ya viongozi

Inapaswa kuwa na mtu anayewaelekeza wengine kuwa na mpangilio; wanaweza kukabidhi majukumu, kuchagua mada za mjadala na kupanga muda na mahali pa kukutania.

2. Fanya utafiti na uwe mbunifu kuhusu mada unazotaka kujadili

Tunapata motisha nyingi kutoka kwenye intaneti na yaliyomo katika habari. Wakati mwingine tunaiomba jumuiya yetu kuhusu matatizo tunayokumbana nayo na kuyajumuisha. Ni burudani kwa kiasi fulani kujumuisha mada nyepesi kuhusu watu maarufu pamoja na masuala yenye uzito zaidi kama vile uhuru wa haki za watoto.

3. Chagua muda na mahali pa kawaida

Pata mahali salama ambako mnaweza kufanyia mijadala. Hii inaweza kuwa katika chumba kwenye maktaba au katika mazingira ya nyumbani kwenu. Jaribu kufanya pawe mahali pa kawaida ili kila mtu aweze kujua jinsi ya kutopaathiri.

4. Panga timu za mjadala na uwe na sheria za kufuatwa

Tuna timu 2 kila wakati ya watu watatu wanaojadiliana dhidi yao. Timu moja inaunga mkono mada fulani huku timu nyingine ikipinga. Kwa mfano, iwapo mada ni kuwa wanafunzi hawapaswi kupewa kazi ya nyumbani, timu moja itaunga mkono wazo hilo huku nyingine itapinga wazo hilo. Kuna muda unaowekwa wa watu kuzungumza – dakika 2 zinafaa - huku watu wengine wakisikiliza.

5. Kuwa na heshima na uwe mcheshi!

Tunahakikisha kila mara kuwa tunaonyesha heshima kwa kila mmoja na hoja wanazotoa, hata kama hatukubaliani nazo. Ni muhimu kusikiliza na kuhimiza kila mmoja ili tuweze kujifunza na kuwa wenye imani.

Baadhi ya mada ambazo utazungumzia iwapo utaanzisha klabu ya mjadala ni zipi?

Share your feedback