Na jinsi ya kuwaepuka walio bandia
Nilipoanza shule ya upili niliwaacha marafiki zangu wengi na kujaribu kuingia kwenye kundi maarufu zaidi. Wasichana maarufu walionekana kuwa na raha zaidi, kupata kuzingatiwa zaidi na kamwe hawakuwa wanadhihakiwa au kudhulumiwa – nilitaka kujiunga nao!
Nilikuwa bado nina ukaribu na rafiki yangu wa dhati Zahra ambaye nilimjua tangu nilipokuwa mtoto, lakini tulizungumza kidogo shuleni. Marafiki zangu wapya hawakupenda mimi kuwa naye. Marafiki zangu wapya walivaa nguo tofauti na walijipodoa zaidi, hivyo nilianza kufanya hivyo pia. Niliacha kuwa kiongozi wa rika shuleni, kwani walisema haikuwa poa na tungekutana tu kwenye egesho la magari baada ya shule badala yake. Haikuwa raha na ya kuvutia kama nilivyofikiri itakuwa.
Marafiki zangu wa zamani walitoa maoni kuwa nimebadilika sana, kwamba yule wa zamani nilikuwa poa na wa kuvutia na kwamba sipaswi kusikiliza hao wasichana wengine. Sikutilia maanani ushauri wao, nilifikiri labda walikuwa na wivu tu kwamba nilianza kuwa maarufu zaidi sasa.
Asubuhi moja kabla ya shule, mimi na marafiki zangu wapya tulikuwa kwenye duka la kona tukinywa milkshake na Zahra akaja nje ya duka. Mmoja wa wasichana aliweka mguu wake juu na kumtega, ambapo ilimfanya Zahra kuanguka na kujimwagia milkshake yake. Aliposimama alikua analia. Nilihisi vibaya sana kwa ajili ya Zahra – nisingesimama na kuruhusu hili kutokea! Nilienda kwake, nikamshikilia na kumwambia angeweza kuvaa t-shirt yangu ya ziada ya michezo kwenye mfuko wangu.
Niliwaambia wasichana ambao walimtega Zahra kwamba walivyofanya haikuwa poa. Kwamba kuwa katili kwa wanafunzi wenzako sio sawa. Na kwamba wanapaswa kufuata mambo mazuri ya kufanya. Sikujali kama kamwe hawangezungumza na mimi tena. Nilijua kwamba hili sio kundi la watu ambalo nilitaka kuwa marafiki nao tena. Hawakuwa marafiki zangu wa kweli.
Marafiki wa kweli husaidia, hukujenga, kukuwezesha kuwa toleo bora zaidi la wewe mwenyewe. Badala yake nilitumia miezi michache iliyopita kuwa toleo baya zaidi la mimi mwenyewe. Nilifurahi kumsimamia Zahra na nilijua kwamba angefanya vile vile kwangu. Nilikuwa na bahati sana kwamba marafiki zangu wa zamani walinisamehe, na sasa tuko karubi kuliko zamani.
Share your feedback