Jinsi mvulana alivyonisaidia wakati wa ajali
Jambo! Jina langu ni Tanya na nina umri wa miaka 16, lakini kila mtu katika mtaa wetu ananifahamu kama “msichana anayecheza kandanda na wavulana”. Ndiyo, mimi ndiyo msichana pekee katika timu ya kandanda ya wavulana shuleni. Watu huniuliza kila wakati nina hisi vipi kushindana na wavulana katika michezo na mimi huwaambia kila wakati; “Basi, wasichana wanaweza kufanya mambo mengi yanayofanywa na wavulana wakipewa nafasi.”
Timu yetu hufanya mazoezi siku tano kwa wiki, kwa hiyo mimi huwa na wavulana muda mwingi wa mapumziko. Tunapozungumza kuhusu timu za kandanda na wachezaji tunaowapenda, sishiriki jambo lingine nao. John tu ndiye tuna uhusiano wa karibu naye. Ni jirani yangu na mama zetu ni marafiki wazuri. Hata hivyo, kuna mambo yanayonihusu ambayo pia yeye hayajui. Wajua, mambo ya wasichana ambayo hata yeye hawezielewa.
Siku moja, tulikuwa tunafanya mazoezo ya mechi dhidi ya timu pinzani. Nilikuwa nimeangazia matayarisho ya mechi ile sana hadi nikasahau kuangalia kalenda yangu ili kujua siku niliyokuwa napata hedhi zangu, na nikaanza hedhi wakati wa mazoezi. John aliona doa lile la damu na akaninong’oneza kwenye sikio, “Tanya, unatokwa na damu”. Nilishtuka na nikakimbia hadi vyumba vya kubadilishia nguo. Lakini sikuwa na nguo wala pedi ya hedhi ya kubadilisha – nilikuwa nimenaswa. Kwa bahati nzuri, mwanafunzi mwenzangu Anna alikuja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na mfuko wa pedi za hedhi na kaptula za kandanda. John alikuwa amemtuma na vitu hivyo aniletee.
Hatimaye nilipopata ujasiri wa kurejea uwanjani, nilikuwa na uhakika John na wavulana wengine watanikejeli. Lakini kwa mshangao, walichoniuliza ni, “Je, uko tayari kucheza kandanda?” Ghafla, niligundua kwamba hedhi sio jambo la kukejeliwa kwa sababu ni kawaida! Kwa hiyo, nilitabasamu na kusema, “Niko tayari kushinda!” Sikuaibikia hedhi yangu tena na pia wewe haupaswi kufanya hivyo.
Share your feedback