Safari ya ndoto yangu

#Imadeit

Jina langu ni Talima. Ninaishi Kenya na shangazi na mjomba wangu. Nimekuwa na ndoto za kuwa mwalimu wa hesabu lakini ndio nifanye hivyo ni lazima ningemaliza shule. Katika muhula wangu wa mwisho nilikuwa nikipata gredi mbaya kwa sababu baada ya shule nililazimika kufanya katika katika duka la shangazi yangu. Ilionekana ni kana mwamba sikuwa na wakati wa kufanya kazi yangu ya nyumbani au kusoma. Darasani ilikuwa vigumu kujibu maswali, hii ilinifanya nihisi ni kama sikuwa mwerevu vizuri. Nikaanza kuhisi vibaya na kutojiamini. Nilipotaka motisha, nililazimika kuwasiliana na dada yangu mkubwa ambaye alinisaidia kurudi njiani.

Aliniambia niwe na imani na nisiruhusu kujishuku kuingilie kati ya ndoto zangu. Ulimwengu unahitaji walimu wa hesabu kwa hivyo siruhusiwi kufa moyo. Aliniamini kwa hivyo ilikuwa wakati wangu wa kujiamini pia. Hivi ndivyo nilivyofanya:

Kujiamini

Kujiamini ndio hatua ya kwanza ya kufanya ndoto zako kuwa kweli. Huanza na mawazo sahihi. Kuwa na matumaini. Endelea kulenga.

Vipaumbele

Niliangalia gredi zangu zote katika miezi 3 iliyopita na nikachagua masomo ambayo nilihitaji kuyazingatia zaidi ili niweze kuyazingatia vizuri. #priorities

Upangaji

Nilitengeneza jedwali la masomo na nikalishiki na shangazi yangu. Ilibidi nipunguze saa zinazotumia dukani ili kusawazisha masomo yangu. Alipoona nilikuwa na mpango alifurahi kunipa muda.

Hatua

Baada ya maandalizi yangu yote kulikuwa tu na jambo moja lililosalia kufanya. Kusoma! Kusoma! Kusoma! Nilifanya kazi kwa bidii na nikajaribu niwezavyo. Nilipokwama niliuliza msaada kutoka kwa watu wangu.

Mwishowe nilipita mitihani yangu yote na nikahitimu! Ndoto yangu ilinipa motisha wa kuendelea. Kuzingatia lengo langu lilinikumbusha kwamba ninaweza. Sasa niko karibu kuwa mwalimu wa hesabu. Iwapo unataka kufanya ndoto zako kuwa kweli, kwanza unapaswa kuamini nguvu na uwezo wako wa ndani. Kisha unda mpango na utekeleze mambo moja baada ya nyingine. Ikiwa msichana kama mimi aliweza kufanya ndoto ikawa kweli, pia wewe unaweza!

Share your feedback