Nyoa nywele kichwani
Siku moja, Anisa alikuwa akijitayarisha kuenda shuleni. Alikuwa akijiikagua dakika ya mwisho kabla ya kuondoka mlangoni alipogundua... nywele zake!
“EEEW! NINA MBA!!!” alipaza sauti.
Ingawa kuwa na mba ni kawaida kama kuwa na chunusi, bado inatia aibu. Unajua habari njema? Si wewe pekee. Kila mtu ana tatizo hili. Mba ni rahisi sana kuangamiza. Hivi hapa ni baadhi ya vidokezo vya kukusaidia:
Sabuni ya bafu
Mba husababishwa wakati ngozi ya kichwa inapotoa seli za ngozi zilizokufa au ikiwa kuna ukuaji zaidi wa kuvu linaloitwa malassezia. Nenda kwenye duka la dawa lililo karibu na ununue shampuu ambayo imetengenezwa kwa minajili ya kukomesha mba. Utagundua kuwa ni rahisi sana kuipata, kwa sababu kama tulivyosema: mba ni ya kawaida kabisa. Osha nywele zako kila siku kulingana na maelekezo ya shampuu. Pia unaweza kuongeza matone kidogo ya mafuta ya mti wa chai kwenye shampuu yako kwa unyevu wa ziada wa ngozi ya kichwa na ufanyizaji wake upya. Unapomalizia kuoga, sugua nywele zako ili kusambaza mafuta asili kutoka kwenye ngozi yako ya kichwa.
Kuwa kawaida
Koma kukuna kichwa chako kwa kukanda aloe vera kwenye ngozi ya kichwa chako kabla ya kutia shampuu. Athari za kupoza aloe vera zitatuliza mwasho. Pia unaweza kutumia mafuta ya zeituni, ikiwa unayo kwenye mkono. Kanda takribani matone 10 ndani ya ngozi yako ya kichwani na ufunike kwa kofia ya kuoga au pakiti ya plastiki usiku mzima. Usisahau kuziosha asubuhi baadaye au kichwa chako kitakuwa na mafuta mengi.
Kile unachokula ndiyo afya yako
Umekutana na zinki? Zinki ni rafiki yako mpendwa mpya wa madini! Vyakula vyenye zinki vinaweza kusaidia kupigana na mba kwa sababu inapunguza kasi ya kubadilika kwa seli za ngozi, pia zinazojulikana kama mba. Tafuta vyakula vilivyo na zinki, kama vile spinachi au mboga nyingine za majani, maziwa na lozi. Sio tu kwamba vyakula hivi vitasaidia kuzuia mba, bali pia ni vyenye manufaa kwako!
Share your feedback