Unataka kujua vile wao huwaza?!
Mimi naitwa Abena. Nilipokuwa mdogo ilitubidi tuhamia mji mwingine ambao babangu alipata kazi. Niliogopa kwenda shule mpya, lakini siku ya kwanza kila mtu alikuwa mwema kwangu na nilipata marafiki wengi sana.
Nina rafiki mmoja shuleni anayeitwa Kofi. Anajulikana sana na yeye hufanya kila mtu acheke. Wakati wa chakula cha mchana, utapata Kofi akicheza kandanda na marafiki zake, lakini huwa tunaenda nyumbani pamoja na kuongea na kucheza hadi jioni. Ni poa sana kuwa na rafiki mzuri kama huyu. Kofi hunisaidia katika kazi za nyumbani, ananichekesha ninapohuzunika, na hunigawia chakula chake cha mchana ninapokuwa na njaa sana.
Siku moja tukiwa shuleni, Kofi akaja kwangu. Alionekana mwingi wa wasiwasi na alitaka tuongee faragha. Nilianza kuogopa pindi tu nilipouona uso wake – Kofi ni mcheshi kila wakati, hivyo kumwona akiwa amekasirika kuliniogopesha. Nilimuuliza shida nini, alinieleza kuwa alipokuwa akitembea kwenye holi alimwona msichana aliyekuwa ameketi sakafuni peke yake. Msichana huyo anaitwa Yvonne na alikuwa mgeni shuleni. Kofi alisema kuwa alitaka kuwa rafiki yake lakini aliogopa. Nikamwambia Kofi ajaribu kumtania ili kumchekesha, kisha amwulize jinsi alivyohisi kuwa katika shule mpya. Nikamwambia asiogope, ni rafiki mzuri kwangu na atakuwa rafiki mzuri kwa Yvonne pia.
Hapo ndipo Kofi aliponieleza kwamba wavulana wengi shuleni wanataka kuwa na urafiki na sisi wasichana kwa sababu sisi ni wajanja na wacheshi, lakini wakati mwingine wanaogopa sana. Kuongea nasiNilishangaa sana kujua hivi ndivyo wavulana hufikiri –kamwe nilijua walitaka kuwa marafiki na wavulana wengine tu, lakini sasa najua wanawapenda wasichana pia!
Inashangaza kufikiri kwamba hakuna tofauti kubwa ya jinsi wasichana na wavulana wanavyowaza!
Share your feedback