Tuna nguvu tukiwa pamoja

Tuko pamoja msichana...

Jambo! Jina langu ni Owami na nina umri wa miaka 16. Nina rafiki yangu mpendwa anayeitwa Mahlo.

Mahlo alipojiunga na shule yetu mwaka wa 2017 katika Gredi ya 8 alikuwa mwenye aibu sana. Alipendelea kukaa pekee yake na kupata chakula cha mchana katika maktaba.

Wanafunzi wengine shuleni walipenda kumfanyia mzaha kwa sababu alikuwa mpweke kila wakati.

Kuna wakati ambapo Mahlo aliombwa na mwalimu kusoma hadithi darasani lakini ilimbidi mwalimu aondoke ili akahudhurie mkutano.

Mwalimu alipoondoka, Mahlo alianza kuisoma. Alisoma maneno kadhaa na kunyamaza. Niliweza kuona kuwa alikuwa mwenye uoga sana lakini wanafunzi wanaoketi sehemu ya nyuma darasani wakaanza kucheka.

Mahlo alinyanyuka na kukimbia kutoka darasani. Nilimhurumia na nikawaambia wanafunzi wanaoketi sehemu ya nyuma darasani kuwa walichokifanya hakikuwa sawa. Kilikuwa kitendo cha ujeuri na wanapaswa kuacha uchokozi kabla sijawaripoti.

Nilimpata Mahlo katika chumba cha kujisaidia akilia. Nilijaribu kumfariji na kumwambia kuwa asijihisi vibaya kuhusu kushindwa kusoma. Ni jambo ambalo hututokea sote. Mimi pia niliwahi kushindwa kusoma wakati mmoja wakati wa kipindi cha dini ambapo nilipaswa kuzungumza. Niliamua kushiriki naye mambo kadhaa ambayo yalinisaidia kunipa imani na kuhakikisha kuwa nimepambana na hali yangu ya uoga wa kuzungumza hadharani.

Nilimwambia kuwa niliamua kuchukulia hali kama hizo kama fursa ya kujifunza. Iwapo niliichukulia kila hali kwa njia nzuri ili maanisha kuwa sikuichukulia kwa wepesi tu, lakini niliiona kuwa hatua ya kujiimarisha mwenyewe.

Nilimweleze pia kuhusu kauli ambayo mimi huitumia kila ninapohisi uoga - na bado ninaitumia kila wiki kanisani! Kurudia kauli “Niko sawa, mtulivu na ninajiamini” kichwani mwangu kwa kweli imenifanya kujihisi hivyo.

Ungependa kujua jambo la mwisho nililomwambia? Kuwa nilikuwa na imani kwake. Tuna nguvu tukiwa pamoja au siyo?

Tulirudi darasani pamoja na ingawaje Mahlo hakuhisi kuwa angemaliza kusoma kwa wakati huo, amefanya hivyo mara nyingi kuanzia hapo.

Na hivyo ndivyo mimi na Mahlo tulivyokuwa marafiki. Tumekuwa pamoja zaidi kuanzia hapo. Tukio hilo lilinifanya kugundua kuwa wasichana wanapaswa kusaidiana. Kuna mambo mengi ambayo tunaweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu ya kutufanya tuwe wenye nguvu - pamoja na kuwa na furaha kwa jumla!

Wakati mwingine huonekana kuwa kuna shinikizo zaidi unapotaka #kuzungumza, lakini unapojua kuwa una uungwaji mkono wa marafiki zako na wanafunzi unaosoma nao darasani, linakuwa jambo rahisi.

Tueleze jinsi unavyowasaidia marafiki zako #kuzungumza katika sehemu ya maoni

Share your feedback