Tulikutana kwa bahati

Ilifungua dunia yangu na kunipa nafasi ya kujifunza

Wasichana na wanawake wengi nchini India wanatarajiwa kusalia nyumbani tofauti na wakiwa nje kwa sababu ya usalama wao. Lakini wasichana wengi zaidi wanapata ujasiri wa kulibadilisha hilo. Hiki ni kisa cha msichana mmoja.

Jina langu ni Meenu, na ninaishi mjini Delhi, nchini India na mama yangu na kaka na dada zangu 5. Baba yangu aliaga dunia nilipokuwa na miaka 5 kwa hivyo mama yangu alitulea peke yake, kwa kipato chake kidogo.

Mama yangu hakusoma, na familia yake ilimlazimisha aolewe alipokuwa na miaka 15. Kila mara alisema kuwa angesoma, angaliweza kutupa maisha bora zaidi. Kwa hivyo alisema ni lazima tusome. Alitusaidia kuendelea kusoma na kutia bidii ili maisha yetu yawe bora zaidi kuliko yake.

Wajomba wangu walihisi kuwa mama yangu alikuwa akiupoteza wakati wake. Walisema kuwa tulipaswa kuolewa ili tuwe shida ya mtu mwingine. Lakini nilimsikiliza mama yangu na kuenda kwenye shule ya bora karibu na makazi yangu duni.

Mama yangu alinishauri kutokujihusisha na wavulana. Alisema kuwa iwapo wavulana wangalinitamani ingalikuwa hatari sana. Watu wakizungumza (au hata kusema uongo) kuhusu kutamaniwa na wavulana, inaweza kuleta aibu kwenye familia yetu — au hata dhuluma kwangu. Nimeiona kwa macho yangu mwenyewe.

Baada ya kuhitimu shuleni nilikaa nyumbani. Niliwajua wavulana wengi katika makazi yangu duni waliosema kuwa wangalinitafuta. Bado, wazo la kuenda nje karibu na wavulana lilikuwa la kutisha. Nilijihisi salama sana nyumbani kwangu mwenyewe ambako ningeota.

Nisingetoka nyumbani kuenda kutafuta kazi. Nilijihisi nisiye na tumaini, nisiye na maana na nilihofia ndoto zangu zisingetimia.

Siku moja mama yangu alinituma kufanya kazi ndogo. Nilipokuwa nikitembea barabarani, nilikutana na mwanamke. Alinialika kujiunga na darasa la kompyuta la wasichana pekee. Nilihofia kwa sababu sikuwa nimewahi kuitumia kompyuta. Pia nilihofia kuenda kwenye kituo cha kompyuta peke yangu, kwa hivyo mama yangu aliniambia niungane na rafiki. “ni wakati wa kuwa jasiri, Meenu,” alisema.

Nilijifunza kuhusu kompyuta, haki za wasichana, na kuifanyia jamii kazi kwa pamoja, na ilinifanya kuhisi vizuri na imara sana. Mafunzo yangu yalipokamilika, nilijitolea kufanya kazi kwenye kituo cha Feminist Approach to Technology kuwafunza wasichana wengine. Nilijihisi kuwa tayari kutuma ombi la kazi ya uuzaji kwa kutumia simu na niliona fahari sana kuja nyumbani kuiambia familia kuwa nimeipata kazi!

Mama yangu alisema kuwa alikuwa na hamu sana ya kuangalia uso wa baba yake alipomwambia kuwa binti yake alikuwa akiletea familia hela! Isitoshe nilipata hela nyingi za kulipia harusi ya dada yangu.

Nilifahamu kuwa sikuwa tofauti na mtu mwingine yeyote. Sihitaji kuhisi kutishika au kujificha pembeni kwa sababu ya wavulana. Nilikuwa na ujasiri wa kujitetea na kuwatetea wasichana wengine wa Delhi. Sauti zetu kwa pamoja zitadai mabadiliko, na isipokuwa Delhi iwe salama zaidi kwa wasichana tutakuwa pamoja.

Share your feedback