Jinsi nilivyostahimili mabadiliko
Jina langu ni Akata na nina umri wa miaka 15. Nilikuwa naishi katika kijiji kidogo hadi pale babangu alipopata kazi mpya na tukapaswa kuhamia jijini. Sehemu yangu fulani ilihuzunika kwa kuwaacha marafiki zangu lakini sehemu nyingine ilipata msisimko kuhusu maisha mapya.
Kuingia ndani ya yasiyojulikana
Niliingia lango la shule yangu mpya na nikasikia kidogo nimezidiwa. Nilikuwa nimetoka darasa la watu 10 hadi 50! Hakuna aliyenifahamisha kwamba watoto wa jijini walikaa na kuvaa tofauti. Baada ya shule niliona kila mtu akibadilisha kwa haraka na kuvaa jinzi na viatu vya kuvutia huku mimi nilibaki na lapulapu na sketi yangu ndefu.
Wasiwasi kuhusu utambulisho
Ilikuwa dhahiri kwa wanafunzi wenzangu kwamba sikuwa nimetoka eneo la karibu. Matamshi yangu yalikuwa tofauti na mavazi yangu vilevile, hivyo watu walinidharau kwa sababu hawakunielewa. Nilihisi shinikizo la kutaka kufanana nao. Ulimwengu unaweza kuwa wa ajabu wakati mwingine. Wanakushauri "kuwa wewe" LAKINI, wakati huohuo wanataka ujaribu na kufanana nao. Wanakushauri "ujieleze na kuzungumza mawazo yako" LAKINI, inapaswa kuwa sawa na yale “wanayokubali". Inachanganya sana.
Mama anisaidia
Mamangu aligundua kuwa sikuwa nabadilika kwa haraka kulingana na maisha ya jijini, kwa hivyo alinieleza siri kubwa. Alinieleza kwamba mara zote watu watajaribu kukulazimisha kuwa mtu fulani na kuishi kwa namna fulani lakini mambo haya si ya muhimu maishani. Cha muhimu ni kuwa na nia njema na kuamini uwezo na nafsi yangu. Je, si hilo na ndilo la ukweli?
Kujiamini wakati wote
Siku iliyofuata nilienda shuleni nikiwa mchangamfu. Sikubadili nguo zangu wala matamshi yangu. Wakati watu walinicheka nilikuwa natabasamu tu kwa sababu nilitambua kuwa mimi ni wa thamani wakati wote. Mimi ni mwerevu na mwenye nguvu na hicho ndicho cha maana!
Mazingira mapya yanaweza kuwa changamoto, lakini usiaibike kuhusu jinsi ulivyo. Jiamini wakati wote kwa sababu kote ulimwenguni kuna mtu mmoja tu kama wewe na hicho ni kitu cha kipekee!
Share your feedback