Kujielezea

Fahamu kwa kweli ‘wewe’ ni nani

Hili limewahi kukutendekea? Siku moja unaamka, unajiangalia kwenye kioo, na kisha… “MUNGU WANGU! MIMI NI NANI?! NI NANI HUYU ANAYENIANGALIA KWENYE KIOO?”

Sote tuna nyakati hizo, haswa wakati wetu wa ujana mambo mengi yanapobadilika. Kwa hivyo, wewe ni nani haswa? Ni nani ‘wewe’ haswa, na nani ‘wewe’ ambaye wakati mwingine unajifanya kuwa wewe? Kutafakari kunaweza kuonekana kwa kutisha, lakini hakuhitaji kuwa hivyo — unachohitaji tu ni kushuhudia mambo mapya.

Jiumbe
Unaweza kuwa yeyote unayetaka kuwa! Ni mambo gani ambayo yanakufanya kuwa mwenye furaha zaidi? Vipaji vyako ni vipi? Ni nini unachoweza kufanya vyema zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Je, wewe ni mkimbiaji mwenye kasi zaidi darasani mwako? Mpishi bora katika familia yako? Msichana mcheshi zaidi katika mtaa wako? Fahamu unachoweza kufanya vizuri zaidi, na unachokipenda, na kisha ukiimarishe — huenda utajifunza jambo moja au mawili kujihusu.

Dewi, mwanafunzi wa shule ya upili mwenye umri wa miaka 15, alituambia kuwa kwa kutambua kwamba alikuwa na kipaji cha sanaa kulimfanya kugundua ubunifu wake. Aligundua kwamba angeweza kujieleza na kuelewa hisia zake kupitia michoro vyema zaidi kuliko maneno. Alitumia stadi za sanaa ili kuwafanya marafiki zake kucheka, kushiriki upendo na familia yake, na kugundua hisia zake binafsi — ziwe za furaha au huzuni!

Wakati wa Kutambua Mambo Mapya, Woohoo!
Bado huna uhakika wa kile unachoweza kufanya bora zaidi? Ni sawa! Njia pekee ya kujua ni kujaribu vitu vingi tofauti kadri ya uwezo wako. Jaribu kufanya kitu kipya kila siku, hata kama kinaonekana kidogo au kisicho na umuhimu — na hata kama unadhani hutakipenda.

Lee, mwanafunzi chuoni mwenye umri wa miaka 20, alituambia kuwa asingeamua kusoma Kiingereza ikiwa asingejiunga na kipindi katika shule ya kati. Hakuwa na mapenzi yoyote ya lugha, lakini marafiki zake wa dhati walikuwa wakisomea kozi na akafikiria angejiunga pia... Ili kuwa tu na muda zaidi wa kutangamana na marafiki zake! Asingewahi kutarajia kamwe, lakini alipenda kujifunza lugha na sasa itakuwa taaluma yake.

Jiamini
Haijalishi unachogundua kujihusu, vivutio na vipaji vyako. Kumbuka kuwa awe ni ‘wewe’, WEWE NI BORA. Hata kama maisha yanaonekana kuwa magumu na ya kuchanganya, unapaswa kujiamini. Usiogope kuwa wewe na kujitangaza huko nje — kila hali ni fursa nyingine ya kujifunaa na kila kosa ni hadithi ya kuchekesha ya kusimulia marafiki zako baadaye. Jiamini, kwa sababu tunakuamini!

Share your feedback